NA TEGEMEO KASTUS
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh, Abbas Kayanda amepokea taarifa ya awali ya zoezi la uthamini iliyotolewa na kamati maalumu iliyounda na Juwamaboe katika vijiji vinavyojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji Tarafa ya Eyasi. Mh. Kayanda amepongeza kamati kwa kazi waliyofanya na kuitaka kutoa mapendekezo ya changamoto zitakazoonekana kwenye tathimini ili isaidie kuondoa malalamiko.
Mh. Kayanda amesema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo katika kikao kilichofanyika Eyasi. Ameelekeza Kamati tendaji ifanye tathimini ya utafiti katika vijiji vya Jobaj, Lakangarer na Malenchand na kamati ialike mjumbe mmojawapo nje ya kamati atakayeshirikiana na kamati katika kufanya tathimini ya maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji katika maeneo ambayo hayakufanyiwa tathimini.
Mh. Abbas Kayanda akiwa katika matukio tofauti wakati wa mkutano.
Mh. Kayanda ameelekeza wajumbe wa Juwamaboe kuanza kufikiria namna wakulima wanaweza kuunganisha nguvu na kuanza kujenga visima vitakavyosaidia katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji Tarafa Eyasi. Akitolea mfano wa kitongoji cha Kambi ya Simba namna ambavyo wameweza kuendelea na kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga visima vya umwagiliaji.
Mh. Abbas Kayanda akiwa katika kikao Tarafa ya Eyasi na wajumbe wa Juwamaboe.
Mh. Kayanda amesema kuna swala la ada za mifereji ya umwagiliaji, ameelekeza viongozi wa scheme kusimamia na kuhakikisha ada zinatolewa katika scheme za maji. Amesema fedha zinazochangwa zitasaidia katika uboreshaji wa ukarabati wa mifereji ya umwagiliaji. Amesema katika ukusanyaji wa ada za mifereji lazima risti zitolewe, amesema wakulima wanapaswa kupewa taarifa ya mapato na matumizi ya michango. amesema lazima Jumuiya ya watumiaji maji iangalie upya kiwango cha gharama zinazotolewa, kama kinaendana na uhalisia wa maisha wanayoishi sasa.
Wajumbe wa kamati ya Juwamaboe wakifuatili kikao cha mkuu wa wilaya ya Karatu.
Mh. Kayanda amehimiza ushirikiano Mzuri kati ya uongozi wa jumuiya (Juwamaboe) na viongozi wa wa scheme katika utendaji wa kazi zao. Amesema kumekuwa na mahusiano yasiyo ya kuridhisha kati ya viongozi wa Juwamaboe na viongozi wa Scheme. Amesema uongozi wa wa scheme unatokana na wananchi na uongozi wa Juwamaboe unatokana na scheme. Hivyo kuna kila sababu ya kuimarisha mawasiliano kati ya viongozi hao na wananchi.
Mh.Kayanda amehimiza swala la kutunza amani, amesema hatuwezi kuishi kwa kufanya visa. Lazima kila mtu awe mtiifu kwa kufuata sheria na kuishi kwa upendo na amani. kumekuwa na watu wanafanya uharibifu wa kuhujumu miundo mbinu ya maji kwa kisingizio cha kudai haki. Amesema yeyote atakayebainika kufanya uhalifu, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa