NA TEGEMEO KASTUS
Mkuu wa wilaya ya karatu MH. Abbas Kayanda ameridhishwa na maendeleo ya miradi ya ujenzi wa miundo mbinu ya elimu iliyojengwa kwa fedha za ndani. Mh. Kayanda ametembelea na kujionea hali ya miundo iliyojengwa na Halmashauri amehimiza walimu kuhakikisha wanatunza miundo mbinu ya madarasa iliyojengwa na kuhakikisha inachangia kuongeza mazingira ya ufaulu.
Mh.Kayanda amesema hayo alipotembelea shule ya sekondari ya Ganako, Banjika Florian pamoja na shule ya Msingi Harraa. Mh. Kayanda ameonesha kuridhishwa na miundo mbinu hiyo ambayo imeonesha kuendana na thamani ya fedha zilozotolewa. Amehimiza walimu kuendelea kuitunza miundo mbinu ya madarasa, ili wanafunzi wapate elimu bora katika mazingira mazuri. Mh. Kayanda amesema kuna mahitaji ya kujenga zaidi miundo mbinu ya madarasa katika shule ya msingi Harraa. Lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya utoaji elimu.
Mh, Kayanda ameojionea ujenzi wa madarasa mawili pamoja na ofisi yaliyojengwa katika shule ya sekondari Florian, na ametembelea na kujionea darasa moja lilojengwa na katika shule ya sekondari ya Banjika na shule ya sekondari ya Ganako.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda (kulia) akikagua darasa shule ya sekondari Ganako
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa