Na Tegemeo Kastus
Wananchi wa kijiji cha Kambi ya simba wamekuwa chachu ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo, wamekuwa vinara katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ikilinganisha na vijiji vingine vya wilaya ya Karatu. Kwa uzalendo walionao wananchi wa kijiji cha Kambi ya simba wanatakiwa sasa wasambaze maarifa hayo kwa wananchi wa vijiji vingine ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akikabidhi gari lililonunulia na serikali kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma katika ktuo cha afya cha Kambi ya Simba. Amesema serikali ikiahidi imekuwa ikitekeleza kwa wakati ahadi zake kwa wakati, gari la wagonjwa katika kituo cha afya cha Kambi ya simba lilikuwa hitaji muhimu.
Mh. Abbas Kayanda kushoto akionesha funguo ya gari la kituo cha afya Kambi ya Simba, akiwa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya (katikati) na Mbunge wa jimbo la Karatu Mh. Daniel Awack
Mh. Kayanda amesema gari kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kituo cha afya kambi ya simba litabaki kwa ajili ya matumizi ya kituo cha afya cha Kambi ya Simba. Amesema lazima uongozi wa kituo cha afya kambi ya simba ulitumze ili lisadie kuboresha huduma za afya katika kituo cha afya cha Kambi ya simba.
picha za gari la afya kituo cha Afya kambi ya simba
Mh. Kayanda amempongeza mbunge wa jimbo la Karatu Mh. Daniel Awack kwa jitihada zake za dhati katika kuleta maendeleo katika jimbo la Karatu. Amesema Mh. Mbunge amekuwa akiweka mbele maslahi ya maendeleo ya Karatu. Amesema hata hivyo uhitaji wa magari ya wagonjwa bado upo kwa kituo cha afya cha Endabash na kituo cha afya Mbuga nyekundu. Amemuomba mbunge kuendelea kulifuatilia jambo hilo ili na vituo hivyo viweze kupata magari ya wagonjwa.
Mbunge wa jimbo la Karatu Mh.Daniel Awack akiliwasha gari la wagonjwa la kituo cha afya Kambi ya Simba
Amesema serikali imeweka nguvu kubwa katika kuimarisha miundo mbinu ya afya, tunakila sababu ya kuipongeza na kuishukuru serikali inayoongonzwa na Mh. Rais Samia Suluhu Hasani. Uwekezaji mkubwa umefanyika katika kituo cha afya Kambi ya simba ambacho kimeweza kukidhi mahitaji ya kutoa huduma. Amewaasa watendaji wa afya kuitunza gari hiyo ili isaidie kuboresha huduma za afya waliyopewa na wala sikufanya kazi nyingine nje ya shughuli za afya.
Mh. Abbas Kayanda akikagua hatua za ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Karatu katika kijiji cha Changarawe
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Kayanda na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Karatu. Ujenzi ambao unaoendelea katika kijiji cha Changarawe, katika ziara hiyo wajumbe wamejionea jengo la kufulia na jengo la dawa likiwa tayari yakiwa yameshaanza ujenzi wa kuta za majengo lakini jengo la utawala likiwa limeshawekwa kenchi kwa ajili ya upauzi.
Ujenzi huo unahusisha jengo la wazazi ambalo litagharimu takribani milioni 55 jengo la mionzi utagharimu takribani million 24, ujenzi wa jengo la dawa million 25 na ujenzi wa jengo la kufulia utagharimu takribani million 19. Ujenzi huo wa majengo hayo unatarajiwa kukamilika mwezi june tarehe thelathini.
Picha katika matukio tofauti wakati wa ziara ya Mh. Kayanda katika hospitali ya wilaya ya Karatu katika kijiji cha Changarawe
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa