• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

DC, AWASHA TAA NYEKUNDU, UPOTEVU WA USHURU WA SAMAKI

Posted on: February 16th, 2020

Kikao maalumu cha kamati ya ushauri wilaya kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri, na kuongozwa na Mwenyekiti Mhe. Theresia Mahongo. Kikao hicho ambacho jukumu lake ni kushauri kilifanya mapitio ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kuridhia kupitisha bajeti hiyo.

Mwenyekiti wa Kikao hicho Mhe. Mahongo amewapongeza watendaji wa Halmashauri kwa kuandaa bajeti bora iliyokidhi mahitaji ya kila sekta. Amesema upangaji wa bajeti mwaka huu umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Makadirio ya bajeti  ya fedha mwaka ujao ni takribani shilingi billion 3.9 tofauti na makadirio ya sasa ambayo ni shilingi billion 3.3. Mhe. Mahonngo amepongeza Halmashauri kwa kufika kiwango cha 50% ya ukusanyaji wa mapato kwa robo iliyomalizika ya mwaka huu wa fedha amesema hiyo ni ishara njema. Amesema fedha za mapato ndizo zinatolewa na serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mhe Mahongo amesema anataka mapato ya mwakani yafike kiwango cha billion 4,  Karatu kuna vyanzo vingi sana vya mapato lakini bado hatuvitumii vizuri. Amesema mathalani ziwa Eyasi watu wanavua samaki kinyemela na kusafirisha lakini hakuna mapato yanayopatikana. Amempa Malekezo Afisa mifugo kwenda kushughulikia changamoto hiyo mapema iwezekanavyo kabla hajachukua hatua kali zaidi.

Mwenyekiti Mhe. Mahongo amesema juzi usiku kikosi kazi kimekamata ndoo 20 jana usiku wamekamata ndoo77 za samaki ambazo hazijalipiwa ushuru. Amesema hawezi kuvumilia upotevu huo wa mapato katika eneo lake. Ameelekeza mashine za malipo kwa njia ya mtandao POS zipelekwe Mang’ola na Afisa tarafa pamoja na Afisa mifugo washirikiane kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali. Njia zote zinazoaminika samaki wanapitishwa wawekwe watu ili kuhakikisha stakabali zinatolewa na watu wanakuwa huru kuendelea na shughuli zao za uvuvi wa samaki.

Maafisa uchumi wa Halmashauri ya Karatu kushoto wakifutatilia kwa makini mapitio ya bajeti ya fedha kifungu kwa kifungu.

Mhe. Mahongo ameelekeza Afisa mifugo kuhakikisha hakuna uvuvi haramu unaofanyika kwa kutumia kokoro. Uvuvi ambao unaharibu mazalia ya samaki  wadogo, amewataka kujipanga na kutoa taarifa za utekelezaji wa maelekezo yake. Lakini pia kuwapa uhuru wananchi kujihusisha na shughuli za uvuvi kwa sababu ziwa limejaa maji na lina samaki wengi kwa sasa.

Mhe. Mahongo ameonesha kusikitishwa na utoro wa wanafunzi katika kata ya Kansay baada ya kupokea taarifa ya watoto 80 ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza katika na shule ya sekondari Kansay. Amemuelekeza mtendaji wa kata ya Kansay kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha watoto hao wamejiunga na elimu ya sekondari. Amesema shule ya Kansay ina madarasa ya kutosha baada ya kukamilika jengo la utawala, amesema awali walimu walikuwa wanatumia  vyumba viwili vya madarasa kama ofisi ambavyo sasa wanafunzi wanavitumia.

Mhe. Mahongo ameasa wananchi kutocheza na elimu, amewaelekeza watendaji wachukue hatua kali kwa wazazi walioshindwa kupeleka watoto shule. Amesema wiki ijayo atakuwa na ziara Kansay kufuatilia  chanzo cha tatizo hilo, ameomba viongozi wa dini kumsaidia kutoa elimu ya ufahamu kwa wananchi juu ya umuhimu wa elimu. Amesema maendeleo hayana lelemama, kwa sasa hatuwezi kueleweka ila baadae ndio tutaeleweka tunachosisitiza. Bila ya elimu tumekwisha tukipata elimu maradhi yatakwisha, umasikini utakwisha, amesema tukicheza nayo tutaumia. Ametoa maelekezo kwa wakuu wa sekondari kuhakikisha hakuna mtoto atakayeshindwa  kwenda shuleni kwa kisingizio cha kukosa sare za shule. Amesema wanafunzi wasio na sare watumie sare za shule ya msingi na waendelee na masomo.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa