Na Tegemeo Kastus
Billion thelathini na saba ni bajeti mpya iliyopitishwa na Halmashauri ya wilaya ya Karatu kwa mwaka ujao wa fedha wa serikali. Bajeti imetenga kiasi cha million mia nne kwa ujenzi wa kituo kipya cha afya ambacho kitajengwa katika kata mojawapo itakayoainishwa na baraza la madiwani.
Hayo yamesemwa katika kikao cha Ushauri cha wilaya ambacho Mwenyekiti wa kikao ni Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda. Amesema maelekezo ya serikali kwa Halmashauri zenye uwezo wa kukusanya kuanzia Bil 1.5 mpaka makusanyo ya Bil 5 kwa fedha za ndani, zinapaswa kutenga bajeti ya kujenga kituo kimoja cha afya kila mwaka wa fedha wa serikali. Amesema bajeti ikiendelea kupagwa kwa kuzingatia vigezo hivyo baada ya miaka mitano kutakuwa na vituo vya afya vitano vitakavyojengwa katika kata mbalimbali.
Amesema serikali inampango wa kuzifanya Halmashauri zijiendeshe zenyewe kupitia mapato yake ya ndani. Ameongeza kusema zipo Halmashauri zimeenda mbali zaidi kwa kujenga vitega uchumi vyake vya mapato kama ofis au hotel ambazo wamezipangisha, amesema ni wakati sasa wa Halmashauri ya Karatu kuanza kubuni na kujenga vitega uchumi. Mh. Kayanda amepongeza wazo la kujenga ukumbi wa kisasa wa Halmashauri kwa ajili ya kuutumia kwenye vikao lakini unaweza kutumika kwenye shughuli nyingine za kijamii.
Matukio tofauti wakati Mwenyikiti wa kamati ya ushauri ya wilaya Mh. Abbas Kayanda akiongoza kikao.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. John Lucian amepongeza serikali ya awamu ya tano inayongozwa na Rais Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa kiasi cha Bilion moja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya na million mia hamsini nyingine kwa ajili ya ukarabati wa zahanati tatu ambazo ni zahanati ya Jobaj zahanati ya Mang’ola Juu na zahanati Huduma.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Ndg. Waziri Mourice ameshukuru baraza la la ushauri la wilaya kwa kupitisha rasimu ya bajeti. Amesema bajeti ya mwaka huu imeandaliwa kwa kuzingatia vipaombele vya serikali ikiwa ni pamoja na kuangalia mahitaji mbalimbali ya Halmashauri kwa mwaka ujao wa fedha.
Kikao kikiendelea chini ya uongozi wa mwenyekiti Mh, Abbas Kayanda.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa