NA TEGEMEO KASTUS
wanafunzi walioshiriki umitashumta wamefanikiwa kupata makombe sita katika michezo volleyball Mshindi wa kwanzawasichana; mshindi wa pili wavulana, mpira wa miguu mshindi wa pili wasichana, mpira wa Handball mshindi wa pili wasichana, Mshindi wa tatu wavulana na riadha mshindi wapili wa jumla na katika medali Karatu imepata medali kumi na tisa ndani yake zikiwepo medali za shaba za dhahabu na silva kulingana na ubora wa mtoto katika mashindano ya mbio.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Ndg. Waziri Mourice amewapongeza wanafunzi hao kwa kushiriki michuano hiyo na kuleta ushindi wa makombe sita na medali. Amesema wanafunzi wamekuwa na nidhamu kubwa katika mashindano jambo ambalo limewasaidia kupata ushindi kwenye mchezo yote waliocheza.
Ndg. Waziri Mourice akipokea kombe (kulia) kutoka kwa mwanafunzi
Ndg. Waziri Mourice kama alivyoahidi hapo awali ametoa kiasi cha 390000 kama sehemu ya kupongeza kila mwanafunzi aliyeshiriki mashindano ya umitashumta. Na amewaasa wanafunzi hao kuendelea kusoma kwa bidiii ili waweze kujiunga na elimu ya sekondari na waweze kushiriki katika mashindano ya Umiseta.
Wanafunzi walioenda katika ngazi ya Mkoa kwa Halmashauri ya wilaya ya Karatu walikuwa jumla ya wanafunzi 86 huku wanafaunzi 9 wakichaguliwa kwenda kushiriki mashindano ya umitashumta kwa ngazi ya taifa. Ndg. Mourice amewapa moyo wanafunzi walioshiriki ili mwaka ujao wajipange vizuri zaidi na waweze kufanya vizuri zaidi ya walipofikia sasa.
Ndg. Waziri Mourice akizungumza na wanafunzi alipowapokea baada ya kutoka kwenye mashindano ya Umitashumta ngazi ya mkoa
Naye Afisa michezo wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Bi,Sara Mollel kwa niaba ya wanafunzi na walimu wa michezo amemshukuru Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya karatu kwa moyo wake wa kimichezo alioonesha wakati wa kuwaaga wanafunzi kwenda kushiriki michezo katika ngazi ya mkoa na wakati wanafunzi waliporudi kutoka kwenye michezo.
Amesema hili ni jambo la kipekeee na limeongeza hamasa na ari kwa walimu na wanafunzi ili kuhakikisha mwaka ujao wanafunzi wanafanya vizuri zaidi. Lakini amewapongeza wanafunzi kwa nidhamu walioonesha wakati wa michezo ya umitashumta, jambo ambalo limewezesha kushiriki michezo kwa amani na utulivu na kurudi nyumbani bila kupata changamoto.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa