Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Mustafa Waziri amewaomba wakazi wa Karatu wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika bima ya afya iliyoboreshwa. Ni vyema watu wakawa na bima kwa sababu itasaidia kuboresha upatikanaji wa dawa, na kuviboresha zaidi vituo vya afya na zahanati kupitia mfuko huo wa bima ya afya iliyoboreshwa ICHF.
Dkt Mustafa amesema Karatu ni wilaya kwanza kuanza mfumo wa bima ya afya iliyoboreshwa ICHF kwa Mkoa wa Arusha. Amesema kwa sasa Karatu imeshanunua simu 32 kwa kila kituo na zitahudumia vijiji vyote 57 vya Karatu kupitia waandikishaji wa bima ya afya. Bima hii imeboreshwa kwa sababu mgonjwa anaweza kuhamishwa (referal) kutoka kituo kimoja kwenda kingine kwa ajili ya kupata huduma nzuri zaidi. Dkt Mustafa amesema kazi za simu ni kwa ajili ya upigaji wa picha kwa wanachama wa ICHF na utumaji wa taarifa na mapato ya fedha kwenye mfumo.
Dkt. Mustafa ametoa wito wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa. Amesema binadamu huwezi kufahamu ni wakati gani unaweza kuugua na kama una fedha au hauna. Dkt.Mustafa amesema ukiwa na bima ya afya iliyoboreshwa inakuwa msaada kwa mwananchi. Bima hii inawezesha wananchi kulipia shilingi 30000 kwa watu sita na kupata huduma ya afya badala ya kutumia mfumo wa malipo ya hapo kwa hapo. Dkt Mustafa amesema Karatu ina wanachi takribani 245000, wananchi wengi wakijitokeza kujiandikisha ili kupata ICHF iliyoboreshwa vituo vya afya vitaimarika zaidi kwa kupata dawa. Fedha za mfuko huo 50% zitatumika kununua dawa katika vituo vya afya lakini pia kuimarisha miundo mbinu ya maji na umeme katika vituo hivyo.
Ndugu Ahmadi Masudi Mratibu wa ICHF wilaya akisisitiza jambo kwa wasimamizi wa ICHF
Dkt Mustafa amesema mwamko wa wananchi kwa ajili ya uandikishaji wa bima ya afya ni mkubwa ila taratibu za kiserikali kwa ajili ya uandikishaji zilikuwa hazijakamilika lakini hivi sasa taratibu zimekamilika kwa ajili ya uandikishaji wananchi kwa ajili ya mfumo wa bima ya afya ICHF. Amesema Upatikanaji wa dawa kwa mwaka 2018 ulikuwa kwa 92.2% amesema kwa mwaka 2019 upatikanaji wa dawa ni 97.9%. Dkt. Mustafa amesema changamoto ya dawa ilikuwa kipindi cha nyuma lakini kwa sasa hakuna changamoto ya upatikanaji wa dawa.
Mratibu wa ICHF iliyoboreshwa ndugu Ahmadi Masudi amesema muitikio wa wananchi katika ICHF utakuwa mkubwa. Ndugu Ahmadi amesema kuongeza wigo wa kupata matibabu kwa mgonjwa baada kupata idhini (referal) ya kupata matibabu kufikia ngazi mkoa ni jambo litakalowavuta wananchi wengi kujiunga katika mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa. Ndugu Ahmadi amesema CHF ya zamani iliweza kuandikisha wananchi wa Karatu kwa 31% amesema wanatarajia kuandikisha wananchi zaidi 50% iliyowekwa kisera.
Ndugu Masudi amesema Halmashauri imepita katika hatua tatu kufikia kutoa semina ya uelewa kwa wasimamizi wa ICHF. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwapata waandikishaji wa ICHF lakini hatua ya pili ilikuwa kununua simu na sasa ni semina ya uelewa kwa wasimamizi wa ICHF.
Wasimamizi wa ICHF katika semina.
Wasimamizi wa ICHF wakifuatilia semina kwa Umakini.
Wasimamizi wa ICHF katika matukio Mbalimbali
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa