Afisa elimu sekondari ametembelea shule ya sekondari Mang’ola na Domel kukagua ufundishaji wa walimu. Katika ziara hiyo Bi. Maina ameambatana na watendaji wa elimu ngazi ya wilaya, na wamekagaua, na kuzungumza na walimu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu taaluma.
Bi. Maina amejionea namna walimu wanavyotekeleza maagizo yake aliyowapa kwa ajili ya utekelezaji. Amesema kila kitu kinawezekana, walimu tuongeze jitihada za ufundishaji wa masomo. Katika ufaulu wa sekondari 32 za wilaya ya Karatu, shule ya sekondari Mang’ola imekuwa ya 16 hivyo ipo katikati kwa kiwango cha ufaulu wilaya. Ngazi ya mkoa imekuwa 135 kati ya shule 226 za mkoa wa arusha. Shule ya Domel imekuwa ya 19 kwa ngazi ya wilaya na ngazi ya mkoa imekuwa ya 155. Amesema watoto wa shule binafsi si kwamba wanauwezo sana kuzidi wanafunzi wa shule za serikali. Ila ni wanafunzi wanaopewa mazoezi ya mara kwa mara darasani jambo linalowapa uwezo wa kujibu maswali katika mitihani ya taifa. Bi, Maina amesema vitu vinavyoangusha shule za sekondari za serikali ni idadi ya ufaulu wa daraja sifuri.
Picha za matukio mbalimbali wakati wa ukaguzi
Naye Afisa elimu Taaluma Bw, Robert Sijaona amesema lazima walimu kuzingatia ujazaji wa maandalio ya kazi uwe mzuri na usiwe wa kuruka ruka. Amesema kukosa vipindi darasani ni kosa baya kitaaluma na linaweza kukufukuzisha kazi. Hiyo ni sawa na kuwauwa wanafunzi kitaaluma. Bw, Sijaona amesema ni vyema walimu wakawa wanapitia notice na mazoezi wanayowapa wanafunzi ili waweze kusahihisha dosari zinazojitokeza. Ameongeza kusema usipo wasahihisha wanafunzi wanaendelea kujifunza makosa na wanajibu makosa hayo kwenye mtihani. Kipimo cha mwalimu kipo kwenye ueledi anaotumia kumfundisha mwanafunzi, na hayo ndio majukumu ya taaluma ya ualimu.
Naye Bi, Brenda Mlay ambaye ni mmoja wa wakaguzi amesema somo la kilimo kwa shule ya sekondari Domel limekuwa na vipindi vingi kuliko uwezo alionao mwalimu kufundisha idadi ya vipindi hivyo kwa wanafunzi. Bi. Brenda ametoa maelekezo kwa uongozi wa shule kuangalia namna ya kupunguza mzigo kwa mwalimu ili aweze kufundisha wanafuzi waliopo kwa ufanisi ili wapate matokeo mazuri. Lakini pia amewahimiza walimu walioajiriwa kuendelea kuhimiza walimu wa ziada katika ujazaji wa andalio la somo na kujaza (class journal) daftari la mahudhurio darasani. Hayo yanaenda sambamba na Ikiwa ni pamoja mpango mkakati uliowekwa na mkuu wa idara ya elimu ya sekondari ya mikakati ishirini na tano ya kuinua kiwango cha elimu wilaya ya Karatu.
Matukio mbalimbali wakati waukaguzi wa walimu
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa