Mpango wa matumizi ya ardhi umezinduliwa katika kijiji cha Dumbechand na mkuu wa wilaya ya Karatu. Uzinduzi umefanyika katika mkutano wa hadhara uliohusisha wananchi na viongozi wa Halmashauri ya kijiji cha Dumbechand.
Uzinduzi huo umenda sambamba na uteuzi wa kamati ya watu nane kutoka kila kitongoji katika kijiji cha Dumbechand itakayoshirikiana na wataalamu kutoka Halamshauri pamoja na UCRT. Kamati hiyo ya wananchi pamoja na wataalamu itafanya mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kusikiliza na kushauriana na wananchi katika kupanga matumizi ya ardhi ya kijiji cha Dumbechand. Zoezi hilo litaanza kwa kutoa elimu kwa wananchi ili wapate ufahamu wa kutosha kuhusu mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Mhe.Theresia Mahongo amesema serikali inafanya mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kupunguza migogoro ya ardhi. Amesema Tanapa wamefadhili mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 17 wilayani Karatu vinavyopakana na Hifadhi ya ziwa Manyara. Mhe. Theresia amesema kwenye tarafa ya Eyasi mpango wa matumizi bora ya ardhi utafanyika kata ya Baray na Mang’ola kwa kufadhiliwa na UCRT.
Mhe. Theresia amesema ili kijji kifanyiwe mpango bora wa matumizi ya ardhi lazima kijiji kiwe kimepimwa, kijiji kiwe na cheti cha ardhi, baada ya kupimwa mipaka yake na ramani yake kuwa imeidhinishwa na kusajiliwa. Amesema sheria ya ardhi ya vijiji no. 5 ya mwaka 1999 na mipango ya matumizi ya ardhi no.6 ya mwaka 2007 kwa pamoja na muongozo wa uundaji wa matumizi bora ya ardhi ulioandaliwa na tume ya taifa ya matumizi ya ardhi. Zimebainisha mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Mhe. Theresia Mahongo akizungumza na wananchi kwenye mkutano Dumbechand
Mhe. Theresia amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi utasaidia kutunza bionuai, na kuimarika kwa miliki za ardhi na matumizi yake. Amewaonya wananchi watakaokwamisha mpango huo wa matumizi bora ya ardhi watashughulikiwa. Amesema kuwazuia wataalamu watakojihusisha na zoezi la kupima ardhi ni kinyume na sheria, ikibainika adhabu yake ni faini sh 30000 au kifungo cha miaka 3 au vyote kwa pamoja. Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi utapunguza ongezeko la watu kuhama hama na kubainsha pia njia za wanyama pori. Mhe. Theresia amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi utapunguza kasi ya kujaa matope kwa ziwa eyasi kunakosababishwa na shughuli za kibinadamu. Amesema kwenye matumizi bora ya ardhi wananchi wataelekezwa hifadhi ya mazingira na namna ya kuzuiwa kujaa kwa matope.
Mhe. Theresia amesema athari za kutokuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi ni kuongezeka kwa migogoro ya ardhi. Amesema kutopima ardhi kuna sababisha soko duni la ardhi lisilo rasmi. Ukiwa na hati ya ardhi ni rahisi kuuza ardhi amesema wawekezaji wanapenda kununua au kuwekeza kwenye maeneo yaliyopimwa. Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi unamsaidia mwanachi mwenye hati kupata mkopo benki. Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi utasaidia kupunguza ukataji ovyo wa miti.
Mhe. Theresia amewaomba wananchi kutoa ushrikiano kwa wataalamu watakaofanya mpango wa matumizi bora ya ardhi. Ameomba wananchi kutoa taarifa sahihi pale madodoso ya kujaza taarifa yatakapo pita. amesema taarifa hizo zitasaidia kujua idadi ya watu na mifugo ili kupanga mpango huo wa matumizi bora ya ardhi. Amewaomba wananchi kutokuwa na hofu pindi wataalamu watakapokuwa wanazunguka mtaani kutekeleza majukumu yao.
Wananchi wa Dumechand wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe.Theresia Mahongo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa