Mafunzo ya kuelimisha wawezeshaji ngazi ya wilaya wa vikundi vya kuweka na kuwekeza yameingia katika hatua nyingine ya ngazi ya kijiji. Wawezeshaji wa ngazi ya taifa kwa kushirikiana na wawezeshaji wa Tassaf ngazi ya wilaya wamefanya mafunzo katika vijiji vya Endala na Baray Khusumay, juu ya namna bora za kuendesha vikundi vya kuweka na kuwekeza.
Muwezeshaji ngazi ya wilaya Ndugu Didas Mkumbwa amesema mafunzo yalilenga kuwaelimisha namna bora yakuendesha vikundi vya kuweka na kuwekeza. Amesema mafunzo ya darasani ya siku tatu na kutembelea vikundi hivyo ilikuwa sehemu ya mafunzo kwa vitendo. Ndugu Didas amesema wamewaelimisha wanavikundi namna bora ya kuweka kumbukumbu katika uwekaji wa fedha namna ya kukopa na kuhakikisha wanawekeza vizuri ili wanakikundi waweze kuinua kipato chao.
Ndugu Didas amesema katika mafunzo hayo kwa wanavikundi wamebaini vikundi vilikuwa vina changamoto ya kutofuata katiba waliyojiwekea kwenye kikundi. Ndugu Didas amesema kuna changamoto ya wanunafaika wa mkopo kuongezea mkopo kabla hajamaliza mkopo wa awali jambo ambalo linamuongezea mkopaji ugumu wa kulipa mkopo kwa wakati. Ndugu Didas amesema wamebaini katika vikundi vilivyopewa elimu kuna tatizo la kuchanganya fedha za mapato na matumizi kwa pamoja jambo ambalo linafanya fedha zionekane nyingi kuliko uhalisia wenyewe na linaleta ugumu katika uwekaji wa kumbukumbu katika vitabu. Ndugu Didas amesema changamoto hizo zinatatulika kwa kuwapa elimu wana vikundi juu ya njia bora za kuweka na kuwekeza.
Mwanakikundi Fausta Joseph wa Endala amesema walikua hawafahamu namna ya kuweka hisa na kuweka kumbukumbu katika kitabu. Bi Fausta amesema kupitia mafunzo hayo wameweza kufahamu maana ya hisa kwamba ni kitu cha kikundi na haikopeshi na akiba ndio wanakikundi wanatumia kukopeshana. Wamefurahi sana Tassaf kwa kuwapa elimu hiyo ya vikundi na wameomba Tassaf waendelee kuwashika mkono ili waweze kufikia malengo.
Wanavikundi wakipewa elimu ya kuweka na kuwekeza
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa