Na Tegemeo Kastus
Kijiji cha Endesh kata ya Baray jana kimepata hati miliki ya kimila baada ya zoezi la kupanga matumizi bora ya ardhi kukamilika kwa kushirikiana na (UCRT ) Ujamaa community resource team. Kijiji kimepewa hati no 22/KRT/ 1 na mgeni rasmi katika sherehe hiyo ya kukabidhi hati ya kimila ya kijiji cha Endesh alikuwa Mheshimiwa Theresia Mahongo Mkuu wa wilaya ya Karatu.
Mheshimiwa Theresia amewapongeza UCCRT kwa msaada wao amewaomba waendelee na mpango wa kupanga matumizi bora ya ardhi. Mpango wa matumizi bora ya ardhi ni mpango mzuri amewaomba watu wanaopotosha zoezi hilo waache. Mheshimiwa Theresia amesema mpango wa matumizi ya ardhi ni mpango wa serikali, Mheshimiwa Theresia Mahongo amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt, John Pombe Magufuli kwa kukubalina na mpango wa matumizi bora ya ardhi. Mpango huu wa matumizi bora ya ardhi utasaidia kuondoa migogoro ya ardhi. Mheshimiwa Theresia amesema katika kijiji cha Endesh wametenga nusu ya eneo kwa ajili ya malisho ya mifugo.
Mheshimiwa Theresia amesema jumapili iliyopita alizindua uogeshaji wa mifugo, amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kujenga josho kwa kushirikiana na wafugaji katika kijiji cha Endesh. Amesema anataka wafugaji wafuge kisasa na mifugo iwe na afya bora. Mheshimiwa Theresia amesema mifugo inakosa soko kwa sababu inakuwa haina hali nzuri ya kiafya. Mheshimiwa Theresia amewaomba wafugaji waache kukwepa kulipa ushuru na kodi mbalimbali kwenye minada. Amesisitiza hakuna nchi itajengwa bila wananchi kujenga tabia ya kulipa kodi, amewaomba wananchi kushirikiana katika kujenga Tanzania
Mheshimiwa Theresia amehimiza wananchi kupeleka watoto shule, amesema shule ya Endesh ipo katika shule kumi zilizofanya vibaya. Dunia ya leo ni elimu, hata kama ni mfugaji utafuga vizuri kama utakuwa na elimu. Mheshimiwa Theresia amesema hatakubaliana na mzazi atakayeshindwa kumpeleka mtoto shule. Amesema amechoka kuona Endesh wanashika nafasi ya mwisho kila mwaka.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa