• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

ENEO LA ARDHI HALIWEZI KUUZWA KWA POMBE

Posted on: July 1st, 2019

Mhe. Mkuu wa wilaya ya Karatu amefanya kikao na wananchi wa kijiji cha Laja na  kusikiliza kero zao zinazo wasumbua. Katika mkutano huo na  wananchi  umehudhuriwa na watendaji kutoka Wilayani, wajumbe wa serikali ya kijiji na wananchi ambao wametoa kadhia na dukuduku kwa mambo mbalimbali yanayowasumbua na hatimae kujadiliwa katika mkutano.

 Mhe. Theresia amemuagiza Mtendaji wa kata ya Kansay kusimamia na kutatua mgogoro wa ardhi wa ndugu Nikodemus Yona. Aliyedai katika kikao hicho eneo la familia kiasi cha hekari sita limechukuliwa na mtu anayedai kwamba aliuziwa na mmoja wa wanafamilia kwa kupewa pombe. Mhe. Theresia amesikiliza malalamiko ya mwananchi huyo na amesema haiwezekani eneo lenye ukubwa wa hekari takribani sita kuuzwa kwa pombe. Amemuelekeza mtendaji wa kata kukutanisha pande zote zinazoshitumiana katika mgogoro wa sehemu hiyo ya ardhi ili tatizo hilo liweze kupatiwa ufumbuzi. Mhe Theresia amemuelekeza ndugu Elikana Lukasi, kupeleka hati za umiliki wa eneo hilo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ifikapo Alhamisi, wakati shauri  linalolalamikwa likiendelea kusuluhishwa katika ngazi ya baraza la kata.

wananchi wakiwa katika Mkutano kijiji cha Laja.

Ndugu Nikodemus Yona ambaye ni malalamikaji wa eneo lililotwaliwa na Ndugu Elikana Lukasi amesema kwenye mkutano huo kwamba wanaonewa. Ndugu Nikodemus anasema eneo hilo lilitwaliwa baada ya baba mwenye eneo hilo kufungwa.  Anasema kutokana na ugumu wa maisha, mama aliyekuwa analimiliki eneo hilo  ambaye ni mke wa mzee aliyefugwa aliondoka katika eneo hilo na vijana wake wa tatu.  ameongeza kusema mama aliyekuwa anamiliki eneo hilo  hakuwa sawa kiakili alipondoka na watoto wake, ndugu Elikana Lukasi ambaye ni jirani katika eneo husika alitumia mwanya huo kulivamia eneo hilo na kuanza kulijenga. Anasema sasa mama huyo amerudi na watoto wake ambao washakuwa wakubwa na wanataka kujenga kwenye eneo lao. Ndugu Nikodemus amesema wamefika ofisi ya kijiji ili kuomba suluhu ya eneo la heka sita na robo tatu linalodaiwa kuuzwa kwa magunia  matatu na pombe. Ameongeza kusema awali waliomba  ofisi ya kijiji kuridhia mgogoro huo usikilizwe na wazee wa kijiji. Ndugu Nikodemus amesema uongozi wa kijiji iliridhia mgogoro huo kusikilizwa na wazee wa kijiji ili kupata muafaka lakini mudaiwa alikataa  kuitikia wito wa kusikiliza lalamiko ya mgogoro huo wa ardhi. Ndugu Nikodemus amesema ilimlazimu kwenda ofisi ya kata na kutoa malalamiko na kumuita mulalamikiwa ambaye aliitikia wito na kutoa hati ambazo anadai aliuziwa kwa shilingi million nane mwaka 1994. Lakini alipoombwa na Mlalamikaji ili kupitia  hati hizo wathibitishe uhalali wake, mdaiwa aligoma. Mdaiwa aligoma kutoa mutasari wa mauziano ya eneo hilo pia ili walalamikaji wajiridhishe. Ndugu Nicodemus amesema hali hiyo ilimfanya kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ambayo msaidizi wa ofisi alimuagiza katibu Tarafa kusimamia tatizo hilo. Ndugu Nikodemus amesema baada ya  kuwasiliana na katibu Tarafa  alimuelekeza kwenda kwa mtendaji wa kata . amesema baada ya  kurudi tena  kwa mtendaji wa kata mlalamikiwa ndugu Elikana hakuonesha tena hati alizodai aliuziwa, badala yake akasema alipewa shamba hilo baada ya kumpa baba mmiliki wa shamba Pombe.

Wananchi wakifuatili Mkutano

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa