NA TEGEMEO KASTUS
Serikali itabuni na kusanifu mradi mkubwa wa maji, ili changamoto ya maji wilaya ya Karatu iondoke. Arusha tumepata maji mengi sana chini ya ardhi, kihaidrolojia maeneo haya karibu na Arusha ikiwemo hapa Karatu na kushuka Singida lazima kutakuwa na maji mengi chini ya ardhi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya maji Profesa Kitila Mkumbo alipofanya ziara ya siku moja wilaya ya karatu. Profesa Mkumbo amefungua mradi wa maji wa Bonde la kwa Tom Karatu mjini kwa kuweka jiwe la msingi. Mradi huo umegharimu million 600.6 mpaka kukamilika kwake na unatoa lita za ujazo 4700 kwa siku na upatikanaji wa maji ni mita 952 za ujazo kwa siku sawa na 33% kwa siku. Amesema tukifanya utafiti kuna uwezekano wa kupata maji mengi sana chini ya ardhi ambayo yatalisha eneo hili. Hiyo ndio mipango mikubwa ya serikali ya muda mrefu kwa ajili ya mji wa karatu.
Pofesa Kitila Mkumbo akimtwika mwanachi ndoo ya maji kama ishara ya kufungua mradi wa kwa Tom
Profesa Mkumbo amesema kisera lazima kuwe na ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali. Sekta binafsi lazima ihusishwe na ijihusishe kikamilifu katika utoaji wa huduma ya maji. Ameongeza kusema uwepo wa Kaviwasu unabaraka zote za serikali. Amepongeza ushirikiano ulipo wilayani Karatu kati ya sekta binafsi na serikali katika kuwapatia wananchi huduma ya maji. Amesema maji yanapaswa kuwaunganisha watu na sio kuwagombanisha amehimiza ushirikiano huo kuendelea kuimarishwa.
Profesa Mkumbo amesema serikali inajiaanda kutekeleza mpango wa muda mrefu wa maji lakini Kaviwasu hawapaswi kuogopa kwamba watakosa kazi. Amesema Kaviwasu hawawezi kukosa kazi, amesema watagawiwa eneo kwa ajili ya kutoa huduma ya maji ambalo wataingia mkataba na mamlaka ya maji. Makubaliano hayo maalumu yatawawekea malengo ambayo wanapaswa kuyafikia, amesema wanafanya hivyo kwa sababu Kaviwasu wameajiri watu wetu. Amesema serikali ya Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli inafurahi watu kupata kazi. Ameongeza kusema lazima serikali iwalinde kwa sababu inawajiri watu na watu hao wanalipa kodi. Amesema jambo la muhimu kwa sekta binafasi ni kusikilza matakwa ya kisheria na maelekezo ya serikali.
Profesa Mkumbo amesema kuna changamoto ya bei za maji wilayani Karatu. Amesema bei ya maji zina muongozo wake. Katika miji bei ya maji inapangwa na watu wa mamlaka ya udhibiti wa sekta ya nishati na maji (Ewura) amesema wao wanapanga na wanaenda wizarani na bei, zikishathibitishwa na wizara zinatoka. Amesema bei zikishatoka hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kwenda juu ya hiyo bei amesema bei ya Ewura ni bei ya mwisho amesema unaruhusiwa kushusha bei lakini sio kupandisha. Watu wa Ewura wako katika mchakato wa kubaini bei sahihi ya maji katika mji wa Karatu. Wanaangalia miundo mbinu yote ya maji, wanazungumza na wadau na wananchi wote na kisha wanapendekeza bei. Amesema wakishapendekeza bei na serikali ikaridhia hiyo ndiyo itakuwa bei ya maji katika mji wa Karatu. Bei hiyo itatumiwa na mamalaka ya maji safi karatu na itatumiwa na Kaviwasu.
Profesa Kitila Mkumbo (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakwanza kulia wakiwa na meneja wa Auwsa (katikati)
Profesa Mkumbo amesema kuna gharama za uendeshaji, amesema lazima wananchi wakubali kulipia bili za maji. Amesema gharama ambazo zimewekwa lazima ziwe chini kuendana na kipato cha wananchi, amesema kama kuna wananchi ambao hawawezi kulipia bili za maji hata lita moja lazima tathimini kubwa ya serikali ifanyike. Kuna utaratibu wa kisera unaoelekeza kuwasaidia wananchi hao kupata maji bure vinginevyo lazima tuchangie huduma za maji ili kuiunga mkono serikali.
Mkuu wa wilaya ya Karatu. Mh. Abbas Kayanda amesema upatikanaji wa maji wilayani Karatu umefikia 56%. Amesema 36% ya sehemu ya maji yanayopatikana Karatu, yanapatikana Karuwasa ambayo ni mamlaka ya serikali. Ameongeza kusema upatikanaji wa maji viijijini kupitia mamlaka ya maji Ruwasa umefikia 64.9% amesema hayo ni mabadiliko makubwa sana.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akimtwika mwananchi ndoo ya maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa kwa Tom.
Mhe. Kayanda amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kwa kupitia wizara ya maji ametoa million 200 kwa ujenzi wa visima viwili vya maji ambavyo ni kisima cha Ayalabe na kisima cha Bwawani. Visima hivyo vikikamilika vitaongeza huduma ya upatikanaji wa maji kwa hali ya juu. Amesema kule Kansay serikali imetoa million 125 kwa ajili kukamilisha usambazaji wa maji kwenye vituo vya kutolea huduma. Mh. Kayanda amesema kuna mradi wa Buger ambao unahitaji fedha kiasi cha million 200 ili maradi nao ukamilike. Amesema mradi ule ukikamilika tutafikia 80% ya upatikanaji wa maji vijijini.
Mh. Kayanda ametoa rai kwa wanachi kutunza na kulinda miradi ya maji ili miradi ya maji iweze kuwa na tija kwa maslahi ya watanzania wote. Amesema haitakuwa jambo la busara kusikia watu wameenda kufungua mabomba au wamekata mabomba. Ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa serikali za vijiji kuhakikisha maeneo ambayo maji yamepita wanahakikisha mabomba yanalindwa na yanakuwa salama wakati wote.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa