NA TEGEMEO KASTUS
Watumishi waliotumia fedha kiasi cha 2,547,000 zilizokuwa sehemu ya ushuru wa mapato mbalimbali ya Halmashauri wamezirejesha. Watumishi hao ni bwana Mbulaingi Wali Mtendaji wa kijiji cha matala ambaye alitumia kiasi cha Tsh. 970,000. Wajumbe wa Halmashauri ya kijiji cha matala walimtaka aitishe kikao ili wasomewe mapato na matumizi ya kijiji lakini alishindwa.
Ndg. Waziri Mourice Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amesema hayo katika kikao cha mwisho cha baraza la madiwani. Amesema mtendaji huyo amefanya hivyo licha ya kila kijiji kufungua account benki kwa ajili ya kuweka fedha za mapato za kijiji. Amesema Mtendaji alikwepa kuitisha mkutano wa Halmashauri ya kijiji kwa sababu alitumia fedha hizo, wananchi walikasirika wakamkamata na wakamuweka ndani. Amesema baada ya kupata taarifa hizo aliagiza Mtendaji wa kata ya Baray aambatane na askari ili wamkamate Mtendaji huyo wa kijiji na wamlete makao Makuu ya wilaya.
Amesema baaada ya kuja Makao Makuu ya wilaya Mtumishi huyo amerudisha kiasi chote cha fedha alichotumia, Ndg. Mourice amesema bado hatua za kinidhamu zinaendelea kuchukuliwa juu yake ikiwa ni pamoja na kupangiwa majukumu mengine ya kiutumishi, amesema tayari wamemuhamisha eneo la kituo cha kazi cha matala na sasa atafanya majukumu mengine makao makuu ya Halmashauri.
Waheshimiwa madiwani wakiwa katika kikao cha baraza
Amesema kuna mtumishi mwingine Raymond Mwasha Afisa mifugo aliyekuwa amepewa mashine ya kukusanyia mifugo na alikuwa anakusanya ushuru wa samaki na ushuru wa sehemu ya geti la samaki. Amesema Afisa huyu alitumia fedha kiasi cha 1,577,000 kinyume na utaratibu baada ya kukamatwa na hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake alirejesha kiasi hicho cha fedha.
Amesema wamemchukulia hatua za kinidhamu Afisa mtendaji huyo amesema kwa sasa hatua wanazochukua ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mashine za ushuru (Pos) mara kwa mara. Amesema kuna wakati watendaji wanazizima (Pos) mashine za kukusanyia mapato na kupokea fedha bila kutumia mashine jambo ambalo si sawa kabisa.
Mkurugenzi ametoa rai kwa watumishi wa serikali kuona utumishi wao kama tunu na wafanye kazi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu. Fedha ukikusanya hakikisha umeipeleka sehemu husika kuepeuka kishawishi cha kutumia; jambo amabalo ni kinyume cha utaratibu, fedha za makusanyo zinapaswa kuingizwa benki
Mkazi wa karatu Fransice Nada amesema swala la watendaji kuchukua fedha zinazokussanywa kwa ushuru ni jambo linalowaumiza wananchi. Amesema fedha hzio zinasaidia kuleta madawa vituo vya afya fedha hzio zinasaidia elimu bure hivyo watumishi kutumia fedha mbichi ni kuwaonea hasa ukizingatia wananchi waanalipa fedha ili serikali isaidie kuwaletea huduma za kijamii katika maeneo wanapoishi.
watendaji wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa