NA TEGEMEO KASTUS
Fedha za mafunzo wa vijana waliyokuwa wanafanya mafunzo ya jeshi la akiba katika kijiji cha Bashay miaka mitatu iliyopita zimerejeshwa. Urejeshwaji wa fedha hizo umefanikishwa kutokana ufuatiliwaji uliofanywa kwa karibu na serikali. Vijana wa jeshi la akiba ambao wamehama makazi na sababu nyingine mbalimbali utafanyika utaratibu maalumu wa kuzitambua familia zao katika ofisi ya kijiji cha Bashay.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akizungumza na askari hao wa jeshi la akiba. Amesema fedha zilizokuwa zinadaiwa ni shilingi million 11 lakini awali zilirejeshwa million 5 na kubakiza kiasi cha million 6 ambazo zimerejeshwa kwa askari hao wa jeshi la akiba katika kijiji cha Bashay.
Mh. Kayanda ametoa rai kwa vijana hao wajeshi la akiba kuendelea kuwa wazalendo kwa nchi yao. Amesema serikali bado inawathamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na jeshi la akiba katika kusimamia ulinzi na usalama. ulinzi na usalama unaanza chini, na ni jukumu la kila mtu, kuimarisha ulinzi kunasababishwa taarifa za watu wema wanaotoa taarifa pindi wanapotilia mashaka miendendo ya watua wasio wema.
Captain Komba kushoto na Katibu tawala B. Faraja Msigwa wakishuhudia zoezi la urejeshwaji wa fedha za vijana wa jeshi la akiba.
Katika hatua nyingine Mh. Abbas Kayanda amezungumza na uongozi wa kijiji cha Bashay, juu ya umuhimu wa kusoma mapato na matumizi kwa wakati bila kusahau kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Amesema Halmashauri ya kijiji ni taasisi kama taasisi nyingine, mfumo wa kiutawala unaanza ngazi ya chini kuanzia kwa mwenyekiti wa kitongoji, amesema ni vyema malalamiko au kero zikaanza kusikilizwa ngazi za chini ili ikishindikana kusikilizwa kwa mwenyekiti wa kitongoji iende kwa mwenyekiti wa kijiji. Utaratibu unaotoa nafasi kwa Halmashauri kijiji kusikiliza kero na zile zinazokuwa nje ya uwezo wa Halmashauri ya kijiji zinapelekwa ngazi ya kata.
Amesema katika vikao vya maendeleo vya kata, mambo mengi ya ngazi za chini yanawasilishwa, na diwani wa kata anapata nafasi ya kuchukua malalamiko na kero zilizoshindikana kutatulika kwenda Halamashauri ya wilaya. Misingi ya mifumo hii ikifuatwa na watendaji wa serikali kila changamoto inayojitokeza ingepatiwa ufumbuzi mapema. Amesema namna mfumo wa Halmashauri ya kijiji ulivyojengwa hauna tofauti mfumo wa Halmashauri ya wilaya. Majukumu ya kamati za Halmashauri za serikali ya kijiji ni muhimu sana katika kuleta msukumo wa maendeleo katika kijiji.
Mh. Abbas kayanda akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya kijiji cha bashay katika kikao cha ndani.
Naye diwani wa kata ya Qurus Mh. Dastan Panga amesema serikali imekuwa ikitoa msukumo mkubwa sana wa kuhamasisha maendeleo kwa wananchi. Migogoro mingi ya ardhi imekuwa ikitatuliwa kwa njia za kiutawala katika ofisi ya mkuu wa wilaya jambo ambalo linaleta faraja kubwa kwa wananchi. Ameishukuru serikali kwa kutumia viongozi wa chini katika kuhamasisha maendeleo na kutatua changamoto za wananchi, jambo ambalo linasaidia kujenga uwezo wa kiutendaji kwa viongozi wa ngazi za nchini.
Mh. Panga ametumi fursa hiyo kumshukuru kamanda wa taaasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru kwa kazi kubwa anayofanya katika kata ya Qurus. Amesema katika mashauri 6 ya ngazi ya kata aliyoyapeleka katika taasisi hiyo tayari mashauri 3 yamefanyiwa kazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halamshauri ya kijiji cha Bashay Raphael Tatock amechukua fursa hiyo kushukuru serikali kupigania na kuhakikisha malipo ya vijana wa jeshi la akiba wanapata fedha zao. Amesema serikali imekuwa karibu na viongozi wa chini ndio maana hata wakati wakilalamika kuomba viongozi wa Tanroad kuweka alama za vivuko kutokana na ajali za barabarani wamepata mwitikio chanya kutoka kwa Tanroad. Serikali imewezesha kupatikana shule shikizi Butiama katika kijiji cha Bashay jambo ambalo lilionekana kuwa na vikwazo vingi hapo awali.
Mh. Dastan Panga diwan wa kata ya Qurus akitoa neno la shukran.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa