• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

“FUNGUKA KWA WAZIRI” MALALAMIKO YA ARDHI ZAIDI YA 250 YASIKILIZWA.

Posted on: March 7th, 2019

Waziri wa ardhi nyumba maendeleo na makazi Mhe. William Lukuvi amefanya ziara wilayani Karatu leo, na kusikiliza kero za wananchi katika uwanja wa Mazingira Bora Karatu. Katika mkutano huo Waziri wa ardhi aliongozana na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu.

Mhe. Lukuvi amesikiliza kero za ardhi za wananchi zaidi ya 250 zilizokuwa zimewakilishwa kwake kupitia kampeni yake mpya inayoitwa "FUNGUKA KWA WAZIRI." Mhe. Lukuvi ametoa maagizo kwa watendaji kundesha zoezi la kukagua watu wasio lipa kodi ya ardhi. Amesema watu binafsi, wenye mashamba makubwa, mashirika na vyama vya ushirika vyenye maeneo makubwa ya ardhi kuhakikisha wanalipa kodi ya ardhi vinginevyo watanyang’anywa.

Mhe. Lukuvi amewaonya watu wenye maeneo makubwa ya adhi kuyatumia kama walivyo omba na sio kukodisha kwa watu wa chini. Amesema atakayebainika kutumia ardhi kwa kukodisha masikini atafutiwa umiliki wa ardhi hiyo hata kama analipa kodi ya ardhi. Amesema kampeni ya nguvu ya kulipa kodi ya ardhi ifanyike nyumba kwa nyumba. Wananchi wote walipe kodi ya ardhi isipokuwa wale waliondolewa kulipa kodi ya ardhi.

Mhe. Lukuvi amesema asilimia tisini ya matatizo ya ardhi Karatu yanatokana na uvamizi wa maeneo ardhi wenyewe kwa wenyewe. Halmashauri wekeni bajeti ya matumizi bora ya ardhi kwenye viijiji ili kuondoa migogoro ya ardhi. Wananchi mlio vijijini pimeni ardhi ili muweze kupata hati za kimila kwa sababu zinakupa ulinzi madhubuti wa eneo lako. Wananchi wanaomiliki ardhi kwa hati za kimila hawatalipa kodi ya ardhi.

Mhe. Lukuvi ametatua mgogoro wa eneo la shule la Ganako na mzee Daniel, ameelekeza Mzee Daniel alipwe fidia na Halmashauri ili aondoke katika eneo hilo. Tunapofanya miradi ya maendeleo ya serikali kuna sheria zinazoruhusu kutwaa ardhi kwa manufaa ya umma. Amesema eneo la mzee Daniel lazima liwe ndani ya shule hivyo atalipwa kutokana na thamani ya ardhi  na nyumba yake ili atoke katika eneo hilo.

Mhe. Lukuvi amesema kuna kesi ya kijiji cha Endala kati muwekezaji ndugu Mroso aliyechukua ardhi ya kijiji cha Endala na kuwa miliki yake. Amesema zoezi la kuhamisha  ardhi ya kijiji kwenda kwa mtu binafsi halikwenda kwa utaratibu unaokubalika. Mhe. Lukuvi  amemuelekeza Ndugu Mroso aliyetwaa ardhi hiyo kurudisha hati ya  ardhi hiyo kesho kwa sababu hakufuata utaratibu mzuri.

Mhe Lukuvi amesema kuna makaburi mawili ambayo yapo kwenye Hotel ya Acacia yalizikwa wakati eneo lile likiwa kijiji sasa ni mji. Makaburi yale yanapaswa kuhamishwa na kuzikwa upya kwenye maeneo mengine ya makaburi kwa heshima. Mhe. Lukuvi amesema makaburi hayo yanapaswa kulipwa fidia, hivyo Halmashauri ya Karatu  itoe notice kwa ajili ya zoezi hilo

 Mhe..Lukuvi amesema kuna watu wamevamia eneo la Mashamba ya Acacia na Tembotembo ambao ni watu maskini, amemuelekeza Mkuu wa Wilaya azungumze na Wakurugenzi wa Acacia na Tembotembo ili watafute namna bora ya kuwabakiza wanachi hao waliovamia eneo hilo


Mhe.Lukuvi akipokea moja ya lalamiko kutoka kwa mwanachi

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa