Na Tegemeo Kastus
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya karatu Ndugu Waziri Mourice amefanya kikao na watumishi wa makao makuu ya wilaya. Kikao ambacho kililenga kutoa uelewa mpana kwa watumishi juu ya virus vya ugonjwa wa corona (COVID-19)
Katika kikao hicho ndugu Mourice amesema swala la corona sio swala la mzaha, amesema kunawa kwa maji ni sehemu ya tahadhari lakini tunashauriwa kupaka mafuta ya kutakasa mikono ili kujiweka katika mazingira ya usalama. Amesema kama kiongozi wa Halmashauri lazima hatua zichukuliwe amesema kuanzia sasa gari lolote linaloingia wilayani lazima wapime joto la abiria kama sehemu ya tahadhari.
Ndugu waziri mourice amesema tumekataza watu kutumia pombe za kienyeji kutokana na mazingira ya unywaji wa maeneo husika. Amesema hata hizi pombe za kawaida ni vyema tukaepuka kunywa, amesema ukinywa akili inabadilika ni vyema tukaacha mpaka hili tatizo litakapopita. Amesema ukifa huwezi ukaenda ukanywa huko utakapokuwa lazima tuchukue tahadhari kubwa katika hili.
Amesema kuanzia sasa hakutakiwi kuwe na msongamano maofisini ametoa maelekezo kwa wakuu wa idara ya elimu sekondari na msingi kuzuia walimu kuja Ofisini kama hakuna shida muhimu. Amehimiza wananchi kununua kitakasa mikono na kupaka ili kujikinga, amesema ukitiliwa shaka karantini iliyowekwa ni sunset au flamingo kwa gharama yako. Mzabuni wa kuleta chakula kwa gharama zako utakapokuwa kwenye Karantini ni Martha wa Sparrow na Teddy wa kimya kimya.
Amesema kwenye usafiri kupanda watu wengi kwenye noah ni hatare, ni vizuri ukapanda magari yenye nafasi ambayo utapitisha hewa vizuri. Amesema wameanza kukamata magari yanayojaza watu kupita kiasi kwa sababu ni hatarishi. Lazima tuzilinde afya zetu kwa sababu afya zetu ndio uhai wako. Amehimiza watu kumuomba mungu ili hili janga liishe kabisa, kila mtu kwa sehemu yake. Amesema kuna utaratibu wa kupata vifaa vikipatikana watumishi wa Halmashauri wataanza kupimwa kila wanapoingia na kutoka ofisin. Amesema lazima kuwe na mtu anasimami zoezi la kunawa mikono kwa kila mtu anayeingia ofisi za Halmashauri. Ndugu Mourice amesema kuna timu ya wilaya imeandaliwa kwa muongozo wa wizara ya afya ajili ya kukabiliana na virusi vya ugonjwa wa corona inayohusisha wataalamu mbalimbali ikiongozwa na mkuu wa wilaya, mtumishi yeyote atakayeitwa kusaidia atoe ushirikiano wa kutosha.
Naye Dkt. Mustafa Waziri amesema jengo la Halmashauri lina wastani wa kupokea watu 300 kwa siku, na hatujui watu wametoka wapi ?? ametoa tahadhari amesema taratibu za kukohoa kwa kuziba mdomo na mkunjo wa mkono ni njia sahihi, lakini pia kufuata taratibu za kunawa mikono kikamilifu. Ameomba watu kufuata maelekezo ya wataalamu, ili kila mtu awe katika mazingira salama.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa