Halmashauri ya wilaya ya Karatu intarajia kufanya mnada wa hadhara wa magari Makuukuu siku ya 25/5/2019. Mnada huo umetangazwa na Majembe Auction Mart na wanatarajia kuuza pikipiki na Mashine inayosaidia kuvuna mazao.
Magari ambayo yanayotarajiwa kuuzwa ni pamoja na gari yenye usajili wa no SM 8008 LANDROVE PUMA ambayo haitembei. Gari yenye usajili wa no. SM 6354 LANDROVER 110SW ambayo haitembei.Gari yenye usajili wa no. T 800 QLN ISUZU TIPPER TON 7 D/INJECTION ambalo halitembei. Gari lenye usajili wa no. SM 21396 ISUZU FIRST TIPPPER ambalo nalo halitembei.
Kuna pikipiki ambazo zitauzwa katika mnada wa hadhara, moja ya pikipiki hizo inausajili wa no. SM 3616 YAMAHA AG 125 ambayo inatembea. Pikipiki yenye usajili wa no. SM 5718 YAMAHA DT 125 ambayo inatembea. Kuna pikipiki aina ya YAMAHA AG 125 ambayo inatembea. Lakini pia kuna mashine yenye no. CW5602 COMBINE HARVEST FIAT AGR ambayo inatembea.
Masharti ya mnada huo mteja ataruhusiwa kukagua siku mbili kabla ya mnada, mnunuzi atatakiwa kulipa 25% ya bei iliyofikiwa kwenye mnada au zaidi na salio la 75% litalipwa ndani ya siku kumi na nne. Endapo mshindi atashindwa kulipa salio la75% ya manunuzi kwa muda uliotolewa atakuwa amepoteza haki yake na mali yake itauzwa tena.
Afisa manunuzi na Ugavi wa wilaya Ndugu Modestus Kasitila amesema bei za bidhaa hizo ni siri na taratibu za kuuza bidhaa zimefuatwa. Mnaada utafanyika katika ofisi za Halmashauri ambazo magari hayo yameweka hivyo ni vyema wateja waje kuona ili wajiridhishe. Amesema wao kama wadau wanataka mtu kununua kitu chenye uhalisia, mathalani kwenye malori amesema licha ya kusema halitembei mteja anaweza kunufaika kwa kupata bodi ambayo anaweza kuweka injini mpya na kuendelea kufanya kazi.
Ndugu Kasitila amesema magari kama Landrover zinazouzwa, zinaweza kufanyiwa ubunifu wa body za landrover. Amesema mathalani kama unataka kuchukua body kwa ajili ya magari ya utalii, unaweza kuongezea viti na likafanya kazi vizuri. Kuna watu tayari wameshaonesha muelekeo wa kutaka kuyanunua magari hayo. Ndugu Kasitila amesema mashine bado inahali nzuri na itakuwa msaada mkubwa kwa mteja atakaye inunua. Amesema hali za pikipiki ni nzuri zinahitaji matengenezo madogo madogo tuu.
Moja ya magari yatakayouzwa siku ya mnada
Moja ya mashine ya kuvuna itakayouzwa siku ya mnada
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa