Mkuu wilaya ya Karatu ndugu. Dadi Horace Kolimba amezindua kitabu cha taarifa ya ushauri elekezi kuhusu mpango mkakati wa miaka mitano wa kuongeza mapato ya halmashauri hiyo kuanzia mwaka 2023 hadi 2028 huku akipongeza watendaji na madiwani wa halmashauri hiyo kuja na mkakati huo.
Mhe Dadi Kolimba ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho cha taarifa ya ushauri elekezi kuhusu mpango mkakati wa miaka mitano wa halmashauri ya wilaya ya Karatu kuongeza mapato huku akiwapongeza watumishi na madiwani kubuni kitabu hicho kwani kitaenda kubadilisha hali za wananchi wa Wilaya hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu ndugu Juma Hokororo kwa niaba ya watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo amewashukuru wataalam hao walioandaa mpango huo kutoka taasisi ya uhasibu Tanzania kwa mchango wao mkubwa katika kuinua mapato ya halmashauri hiyo
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karatu dokta John Lucian Mahu amesema wataalam hao watasaidia kukuza mapato ya halmashauri hiyo hasa katika sekta ya utalii na kilimo cha vitunguu katika bonde la Eyasi.
Hata hivyo, Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Wamekiri kuwa kitabu hicho kitakua kiongozi katika kutambua namna bora ya kukusanya mapato katika Halmashauri hasa katika yale maeneo ambayo hawajawai kukusanya mapato au hata yale wanayo kusanya wataboresha zaidi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa