Kikao cha wadau wa afya kilichodumu kwa muda wa siku mbili kimemalizika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Kikao hicho kimefungwa na mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Jublate Mnyenye.
Kikao hicho cha wilaya cha wadau wa Afya na mapambano dhidi ya ukimwi, kimejikita katika kujadili taarifa za afya na upimaji wa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi. Lakini pia mikakati imara ya kuhamasisha wananchi kujitokeza na kupima ili kujua taarifa za hali zao za afya. Mkakati ukiwa ni kufikia 90% ya upimaji wa wagonjwa, na 90 % ya wagonjwa waliopimwa wandikishwe sehemu kwa ajili ya matibabu na 90% ya wagonjwa waliopimwa waanze matibabu.
Mhe. Mnyenye amewapongeza wadau hao wa afya kwa kukutana, amesema kikao hicho ni muhimu sana na nilazima kijumuishe wadau wote wa afya. Amesema kwa wale wadau afya ambao hawataki kushiriki hatua kali zichuliwe dhidi yao. Amesema kuliko kuwa na jino bovu ni bora ubaki na pengo. Kama tuna mdau halafu kila kitu anaficha ficha kuna faida gani ya uwepo wake kwetu??
Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Mustafa Waziri amesema sasa watajikita katika utengenezaji wa Mabanda kwa ajili ya kupima afya kwenye Minada sambamba na kukusanya damu salama. Lakini pia kuwahimiza watu kujiandikisha ICHF iliyoboreshwa.
Dkt. Mustafa amesema moja ya maazimio ni kuboresha ICHF, tutaanza na mkakati wa kuelimisha wanufaika wa Tasaf kujiunga na ICHF iliyoboreshwa. Lengo likiwa ni kuwahamasisha wananchi wengi kujiunga lakini pia kupata mabalozi ambao watakaoeleza wananchi wenzao juu ya manufaa ya kujiunga na ICHF.
Dkt. Mustafa amesema azimio la pili la kikao cha wadau wa afya na mapambano dhidi ya ukimwi, ni kuita wadau wengine wa afya ambao hawakuhudhuria ili kufahamu utendaji wa shughuli zao za afya katika wilaya ya Karatu. Kabla ya kuanza kuwachukulia hatua kwa utoro wa kutohudhuria vikao halali vya wadau wa afya.
Dkt. Mustafa amesema azimio la tatu ni kusambaza condom katika nyumba za wageni, ikiwa moja ya jitihada za kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Dkt. Mustafa amesema azimio la nne ni kuwapima Dada poa katika matukio ya kuwakamata yatakayofanyika. Lengo pia ni kufahamu takwimu za idadi ya maambukizi katika wilaya ya Karatu. Lakini pia kupima kwenye Baa na Hoteli kubwa kupata idadi kamili ya watu waliojitokeza kupima afya kabla ya kikao kingine cha wadau wa afya.
Dkt. Mustafa amesema azimio la tano ni kuwelimisha wananchi kupitia vikao vya kijiji juu ya manufaa ya wananchi kujiunga na ICHF. Lakini kuwaelimisha wananchi juu ya maswala mbalimbali ya afya yanayohitaji ufafanuzi ili kuwaongezea uelewa.
Wadau wa afya wakisikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Jublate Mnyenye.
wadau wa afya wakimsikiliza Mhe.Jublate Mnyenye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa