Na Tegemeo Kastus
Wilaya ya karatu hatutaki ufaulu wa daraja sifuri katika mtihani ya kitaifa wa kidato cha nne na mitihani wa kidato cha pili. Ufaulu wa mwanafunzi unaanza kwa mwanafunzi kupata ufaulu wa alama D mbili ni jambo linalowezekana kufanyika.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa akikabidhi viti 75 na meza 75 vilivyotengenezwa na wazazi katika kukabiliana na changamoto za upungufu wa madawati. Meza na madawati pamoja na ukarabati wa madarasa mawili yamegaharimu million 5250000, amesema wazazi wa vijiji vya kilimamoja, huduma na chemchem wamefanya hivyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya msingi na mpaka kidato cha nne kwa sekondari.
Mh. Abbas Kayanda akwa katika picha ya pamoja na wanafunzi, walimu na uongozi wa serikali ya vijiji vitatu baada ya kukabidhi madawati kwa uongozi wa sekondari Kilimamoja.
Mh. Kayanda amesema faraja pekee wanayopata wazazi ni kuona vijana wao wanafaulu, na wanaendelea na elimu ya juu. Amesema wanafunzi wametengenezewa mazingira mazuri zaidi ya kusoma lazima sasa walimu waongeze jitihada katika kuondoa daraja sifuri. Ameongeza kusema kama ufaulu utaongezeka hata shida ya ujenzi wa jengo la utawala inaweza kutatulika. Wazazi watapata moyo wa kuendelea kujitoa kwa ajili ya watoto wao, ameomba walimu kuongeza ufuatiliaji wa wanafunzi kwa kushirikiana na wazazi pindi wanapobaini changamoto za mtoto katika maendeleo yake ya kitaaluma.
Mh. Kayanda amepongeza uongozi wa serikali ya kijiji kwa kusimamia maagizo ya serikali ya kukarabati na kumalizia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa. Amesema ukarabati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa umezingatia vigezo na umetoa picha nzuri kwa serikali na umesaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa.
Mh. Kayanda ametumia fursa hiyo kuwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo ili kupata matokea mazuri.a Amesema taifa linauhitaji wa wataalamu mbalimbali na wataalamu wanajengwa kutoka shuleni, ametoa rai kwa wanafunzi kuweka mkazo mkubwa katika masomo.
Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Africa Galleria baada ya kuwakabidhi madawati
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda ametembelea shule msingi ya Africa Galleria na kukabdidhi madawati 65 yaliyojengwa muwekezaji wa Africa Gallleria. Madawati hayo yamesaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika shule hiyo ya msingi. Amempongeza muwekezaji Africa Galleria kwa kukumbuka kurudisha kwa jamii, jambo ambalo linazidi kujenga mahusiano chanya na jamii.
Akiwa katika shule ya Msingi Kainam Rhotia Mh. Kayanda amekabidhi madawati 48 ambayo yamejengwa na kukarabatiwa na wazazi katika shule hiyo. Mh. Kayanda amepongeza wazazi kwa kuwa na mutikio chanya na kuhamasishana katika shughuli za maendeleo lengo likiwa ni kusaidia taasisi zinazozunguka maeneo yao.
Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wanafunzi wa Kainam Rhotia baada ya kuwakabidhi madawati
Sambamba na kutembelea miradi ya elimu Mh. Abbas Kayanda ametembelea zahanati ya Kainam Rhotia ambayo imepewa kiasi cha million sita kwenye fedha za mfuko wa jimbo kwa ajili ya ujenzi wa kichomea taka, ukarabati wa maabara na ujenzi wa jengo la choo. Mh. Kayanda ameelekeza uongozi wa Halmashauri ya kijiji kuepuka matumizi mabaya ya ununuaji wa vifaa vya ujenzi. Amesema kumekuwa tabia ya watendaji kuweka gharama kubwa za Quotation za miradi, gharama ambazo haziendani na bei ya uhalisia ya ujenzi wa jengo. Ameelekeza wataalamu kujiridhisha thamani ya bei za ununuaji wa vifaa vya ujenzi. Ameeleza uongozi wa kijiji kusimamia na kuhakikisha huduma ya nishati ya umeme inaunganishwa katika zahanati hiyo mapema.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo diwani wa kata ya Rhotia Mh.Marsel Magasi amesema ziara ya mkuu wa wilaya imezidi kuwapa hamasa ya kusimamia shughuli za maendeleo. Amesema ili kata iwe na uwezo wa kufanya shughuli zake lazima kuwe na ushirikiano wa viongozi wakijiji katika kila eneo ambao watasaidia kuibua na kutatua changamoto zitakazowasilishwa katika ngazi ya kata.
Mh. Magasi ameshukuru wananchi wa kata ya Rhotia kwa kujitoa katika kutekeleza shughuli za maendeleo. Amesema Zahanati ya Kainam Rhotia itakapokamilika itasaidi kusogeza huduma za afya karibu zaidi. Ameomba uongozi wa kijiji cha Kainam Rhotia kuweka nguvu katika ujenzi wa zahanati ili uweze kukamilika kwa wakati.
Mh. Abbas Kayanda akikagua maendeleo ya ujenzi wa choo katika zahanati ya Kainam Rhotia
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa