Na Tegemeo Kastus
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Technolojia Dk. Avemaria Semakafu amefanya ziara katika shule ya sekondari ya Florian wilayani Karatu. Katika ziara hiyo amejionea kazi zinazofanywa na shirika la world education initiative (WEI) katika kunyanyua taaluma ya mtoto wa kike.
Dkt. Avemaria Semakafu amewaambia wanafunzi wa shule ya sekondari Florian kwamba wote wanaoacha shule siyo kwa sababu ya mimba au kuolewa. Amesema kunawatoto wa kike wanaacha shule kwa sababu ya mila, wengine kwa sababu ya umbali mrefu na shule ilipojengwa.
Dkt. Semakafu amesemba wanafunzi wanaogopa mimba kuliko hata corona, amesema maisha yapo ili tuyafurahie. Amesema mwanafunzi atafurahia maisha yake ya shule kama hata jihusisha na mapenzi. Amesema ukianza kujihusisha na mapenzi; kuacha ni kazi, ameomba wanafunzi kujifunza kwa mabinti wenzao waliokatishwa masomo kwa sababu ya ujauzito. Amesema mtoto wa kike akisoma anakuwa na msimamo, amesema ni vyema wanafunzi wa kike wakawa na msimamo.
Dkt Semakafu amesema Tanzania inaelekea uchumi wa viwanda, je Florian mmejianda vipi ? amesema unapozungumzia uchumi wa viwanda unaongelea Mainjinia, Madaktari, Mafundi wasanifu, watu waliobobea kwenye mambo ya uchumi. Amesema kwa matokeo aliyopewa ya kidato cha sita na matokeo ya kidato cha nne hayaridhishi. Ameomba wanafunzi kutumia klabu zilizoanzishwa kuinua ufaulu wa kitaaluma. Amesema lazima Florian ijipange kutoa watu watakaosaidia kujenga uchumi wa viwanda.
Dkt. Avemari Semakafu (aliyekatikati) akizungumza jambo na watendaji wa idara ya elimu wilaya ya Karatu
Dkt. Semakafu amesema mathalani katika ujenzi wa standard Gauge alioutembelea Ma-project Meneja wa mradi wa reli kutoka Dodoma mpaka Makutupora ni mdada na Makutupora mpaka Mwanza Project Meneja ni mdada wa kitanzania. Katika ujenzi wa Mahandaki, sehemu ambazo treni itatoboa mlima na kupita chini ya milima kwa baadhi ya maeneo, amesema anayesimamia mradi huo injinia mkubwa ni dada mwenye asili ya kituruki. Ameomba mabinti wa kike wa shule ya wasichana ya Florian kuhamasika na kusoma kwa bidii ili waje waisaidie nchi.
Dkt . Semakafu amesema Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipoamua kuondoa vikwazo katika elimu msingi na sekondari mpaka kidato cha nne kuwa bure alikuwa anamaana mwanafunzi asishindwe kwenda shule kawa sababu ya kukosa ada. Mwanafunzi asishindwe kwenda shule kwa sababu kuna mchango wa taaluma shuleni ambao ameambiwa achangie. Amesema Wanafunzi watasema asante ya aina gani ?? Amesema kazi ya mwanafunzi ni kusoma na kufaulu, amesema awali wanafunzi walikuwa wanasoma wanakosa shule au madarasa ya kusomea. Amesema lakini kwa Mhe, Rais Dkt. John Pombe Magufuli lazima madarasa yajengwe, ameuliza wanafunzi wa Florian wanatakwa wapendwe vipi ??
Amesema wanafunzi lazima wajipange kufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza ili hata wakianguka upate daraja la pili. Dkt. Semakafu amewaasa wanafunzi kuacha kupitia njia za mkato, ametumia fursa hiyo kuwaasa walimu kuacha kujihusisha kimapenzi na wanafunzi amesema hilo ni jambo la aibu na linachangia kudidimiza elimu mashuleni. Amewambia walimu tunahitaji kuwasaidia vijana wetu, na tutawasaidia kama hatutajihusisha na vitendo vya kuzalilisha wanafunzi. Amesema wizara ya elimu haitaki mimba shuleni, haitaki mdondoko wa wasichana kutoka kwenye elimu, kampeni kubwa sasa ni kujenga mabweni kwenye shule za sekondari.
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Technolojia Dkt. Avemaria Semakafu (aliye katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Florian.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa