Kikao maalum cha baraza la madiwani kwa ajili ya kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali ya hesabu za Halmashauri za mwaka wa fedha ulioisha tarehe 30/june/2018 kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo amepongeza wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu kwa kupata hati safi. Amempongeza sana Mkaguzi mkuu wa serikali kwa kazi nzuri aliyoifanya, na kubaini matatizo mbalimbali. Amesema ameagiza Halmashauri zote wapate taarifa za kibanki; Manunuzi, kwa Mkaguzi wa ndani, mara baaada ya kukamilisha mabaraza yote mkoa mzima, ili kwa kushirikiana na Menejimenti ya mkoa ziweze kufuatiliwa. Amesema taarifa hizo pia zitasaidia kufanya mlinganisho kwa kushirikisha wakaguzi wa serikali ili kuongeza umakini na kuondoa kutojiruadia kwa dosari zilizojitokeza. Amesema hoja nyingi za Halmashauri inazopata ni uzembe, inawezekana vikao vya maamuzi vya Halmashauri havifanyi kazi vizuri au kamati ya fedha ya Halmashauri haifanyi kazi vizuri. Amesema ni imani makosa ya namna hii hayatajirudia tena, na dosari zilizojitokeza zitapatiwa ufumbuzi kwa wakati.
Awali katika kikao hicho hoja ya vifaa vya ujenzi vilivyolipiwa lakini havikuwasilishwa Halmashauri vienye thamani ya sh.79,542,000 uliohusisha Msambazaji Anatoly construction ilibainika wakati wa ukaguzi uliofanywa na mkaguzi mkuu wa serikali. Ushauri wa mkaguzi Mkuu wa serikali kwa Halmasahuri ilikuwa kuimarisha uthibiti wa mifumo yake na pia fedha yote inayolipwa kwa mzabuni irudishwe kwa Halmashauri. Hivyo kamati iliona kuna udhaifu katika manunuzi ya umma. Hivyo Mhusika wa kitengo cha manunuzi kuandikiwa barua ya onyo yenye kumbukumbu na. KDC/DED/Cs.1/8/VOL.1V/30 na ilielekezwa kufuata sheria za manunuzi ili kuzuia hoja kama hizo. Hatua hizo zlichukuliwa baada ya kamati ya ukaguzi kubaini vifaa ambavyo vimeshalipiwa kutoletwa kwa ajili kukamilisha ujenzi wa soko.
Awali kamati ya fedha ilijadili hoja hiyo na kutoa maamuzi baaada wiki moja vifaa vilivyokuwa vimekosekana viwe vimeletwa na kuweka stoo, lakini mpaka kikao kinafanyika vifaa havikuwa vimeletwa stoo. Mkurugenzi mtendaji ndugu Waziri Mourice ambaye alikuwa Khatibu wa kikao hicho, alikiri udhaifu katika utendaji wa kulishughulikia swala hilo. Amesema ndani ya wiki moja vifaa vyote vitakuwa vimeshaletwa kutoka kwa msambazaji, na kamati ya fedha ya Halmashauri itapitia kuhakiki vifaa hivyo.
Kaimu mkaguzi wa nje ya Mkoa Monica Mushi amesema swala hilo linaleta utata baada ya kitengo cha manunuzi kutoa fedha zote kwa ajili ya kununua vifaa kwa muuzaji. Amesema ilitarajiwa baada ya kutoa kiasi chote cha fedha vifaa viletwe vyote lakini kitendo cha kununua halafu unaacha vifaa kwa msambazaji, sisahihi kwa sababu anaweza kukataa kwa kusema ameshakuuzia na hana vifaa hivyo tena. Amesema udhaifu wa kuonesha vifaa vimenunuliwa kwenye nyaraka halafu vifaa vikaachwa kule ndio unaoleta hoja. Amesisitiza siyo lazima kulipa fedha nyingi katika kununua vifaa vyote, bado tunaweza kununua vifaa kidogo kidogo kadri ya mahitaji.
Hoja nyingine ambayo ilileta mjadala kwa Halamashauri wakati wa kikao ilikuwa, ni mapungufu ya katika usimamizi wa vibanda vilivyo katika eneo la mnada. Mkaguzi wa serikali alibaini vibanda hivyo kushindwa kukamilika kwa wakati, lakini pia kiwanja kugawiwa kwa zaidi ya mtu mmoja na kwa watu ambao hawakuwa kwenye orodha. Mkaguzi wa serikali alibaini baadhi ya wapangaji wa vibanda wamemilikishwa na kugawiwa watu wengine bila kuwa na makubaliano na Halmashauri.
Menejimenti ya Halmashauri katika majibu yake kwa mkaguzi ilisema kulikuwa na makosa ya ya uhandisi kujirudia kwa majina na ramani na mikataba ya wamiliki. Hivyo uhakiki unaendeelea ili kuondoa tatizo la majina ya wamiliki kujirudia. Menejimenti ya Halmashauri imedai waliopewa vibanda walipewa kutokana na maombi ya malipo yaliyofanyika baada ya kupata vibanda. Menejimenti ya halmashauri imedai mkataba haumruhusu mmiliki kumilikisha mtu mwingine bila makubaliano ya Halmashauri.
Baraza limeamua watu waliopewa vibanda na kujenga mpaka kwenye hatua ya kuweka paa na watu walioanza kujenga msingi wapewe muda ili waweze kukamilisha ujenzi wa vibanda hivyo. Baraza limebaini vibanda 109 viko katika hatua ya kuweka paa, na wamepewa muda wa mwezi mmoja wawe wamemaliza kujenga vibanda hivyo. Vibanda 323 viko katika hatua ya kujenga msingi baraza limeamua kuwapa muda wa miezi miwili kumaliza ujenzi wa vibanda hivyo. Baraza limeamua wamiliki wa vibanda 122 ambao hawajaendeleza wanyang’anywe umiliki wa vibanda hivyo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa