Ziara ya mkuu wa mkoa wa arusha Mhe. Mrisho Gambo imeendelea wilayani Karatu, katika ziara yake ametembelea eneo lilokuwa la kutupa taka katika soko kuu la Karatu. Amejionea hali ya mazingira na kutoa maelekezo kwa watendaji.
Mhe. Gambo amemuelekeza Meneja wa Tarura wilaya kufungua barabara iliyokuwa imefungwa katika eneo hilo baada ya kutengwa kama kituo cha kukusanyia taka kupeleka jalalani. Amesema wanaoweka uchafu ni watu wa soko utaratibu wa sasa kila mfanyabiashara awe na chombo au kifaa cha kuhifadhia uchafu wake mpaka gari la taka linapopita. Ameomba watu wa soko kulinda watu wasitupe taka katika eneo hilo na ni lazima wafanyabishara waoneshe nia hiyo kwa vitendo. Mhe. Gambo ameelekeza watu wa Tarura kuvunja ukuta katika eneo hilo na kufungua barabara iliyokuwa imefungwa.
Mkurugenzi mtendaji Ndugu Waziri Mourice amesema eneo hili lilikuwa sehemu ya kukusanyia taka, amesema mpaka jion eneo hilo la kutupa taka litakuwa limeshabadilishwa matumizi yake na kufungua barabara iliyokuwa imefungwa. Amesema wafanyabishara hawataweka tena uchafu katika eneo hilo na baadala yake watasubiri gari la taka kuchukua taka zinazozalishwa katika eneo la soko.
Hili ndio eneo ambalo jalala limeondolewa katika eneo la soko kuu la Karatu.
Injinia Julius Kaaya amesema kama Mkurugenzi mtendaji akiliondoa jalala hilo sokoni, wao kama wakala wa barabara vijijini watafungua njia hiyo. Injinia Kaaya amesema kumekuwa na uvunjifu wa sheria katika kutumia eneo ambalo limezuiwa kisheria kufanya shughuli za biashara. Amesema kwa sababu mkurugenzi mtendaji ameliondoa jalala katika eneo la soko. Hivyo Tarura watafungua barabara hiyo na kuanza kutumika .
Mkazi wa eneo hilo John Tipe amesema eneo hilo lilotegwa kama jalala ni kweli ni eneo ambalo barabara inapita kuzunguka soko la Karatu. Amesema uchafu unaokaa eneo hilo unaleta adhaa ya harufu mbaya kwa wafanyabishara na wananchi wanaozunguka eneo hilo. Ndugu Tipe amesema eneo hilo kwa nyuma kuna eneo lake la biashara ambalo awali lilikuwa ndio sehemu ya kukusanyia taka. Lakini kwa sabababu alilipangisha eneo lake kwa wafanyabishara aliamua kuondoa jalala hilo kwenye eneo lake na baadae jalala likawekwa katika hifadhi ya barabara ambayo ilikuwa imefungwa. Ndugu Tipe amesema kufungwa kwa barabara hiyo kumesababisha hata magari makubwa yanayokuja kupakua mzigo kupata shida ya kugeuka katika eneo hilo. Ameomba jalala hilo kuondolewa katika eneo hilo kwa sababu wakati jalala hilo linawekwa walipinga lakini nguvu kubwa ilitumika kuliweka jalala katika eneo hilo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa