Na Tegemeo Kastus
Siku ya wanawake ni siku muhimu sana kwa ustawi wa vijana wetu wa kike, lazima tufanye maandalizi kwa kuanza ngazi ya kijiji kata na kilele kifanyike katika ngazi ya wilaya. Maadhimisho yalenge kujenga uelewa wa pamoja kati wanawake na vijana wa kike walio bado shuleni.
Hayo yaemesemwa na Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Karatu Mh. John Lucian wakati akizungumza katika kilele cha siku ya wanawake kilichofanyika katika Uwanja wa mazingira Bora Karatu. Amesema malengo ni kumjengea uwezo wa kimaadili mama wa leo na mama wa kesho, kwa kuanzia katika ngazi ya kijiji mpaka kufikia ngazi ya wilaya.
Mh. John Lucian akitoa salamu katika maadhimisho ya siku ya wanawake
Mh. Lucian amesema Halimashauri haitatoa mikopo ya upendeleo, itaendele kusimamia utoaji mikopo2% kwa walemavu, 4% kwa vijana na 4%kwa wakinamama. Lazima tuchukue hatua za kuwawajibisha watu ambao hawataki kurejesha fedha za mikopo. Amehimza watendaji kutoa mikopo kwa kuzingatia usawa bila kupendelea maeneo.
Matukio tofauti wakati Mh. Lucian akitoa salamu
Naye afisa maendeleo ya Jamii wilaya ya Karatu Bi, Adelaida Shauri akitoa salamu za shukrani, amesema Halmashauri imetoa kiasi cha million 120 kwa vikundi vya kinamama vijana na wazee 96. Amesema changamoto kubwa idara ya maendeleo ya jamii inakabiliana nayo ni baadhi ya wanawake wanaopewa mikopo kushindwa kurejesha kwa wakati. Amesema serikali imeunda sheria mpya ya mwaka 2019 inayomuwezesha Afisa sheria wa Halmashauri kuwashitaki Mahakamani watu wanaoshindwa kurejesha mikopo isiyo na riba ya Halmashauri. Amesema kwa kupitia sheria hiyo kikundi kitakachoshindwa kurejesha fedha hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Amesema kama watu wanaopewa mikopo wangeweza kuirejesha kwa wakati Halmashauri ingeweza kutoa kiasi cha million 300 kwa ajili ya mikopo isIyo na riba kwa wanawake vijana na walemavu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa