Na Tegemeo Kastus
Ujenzi wa nyumba mbili za watumishi na jengo la magereza ya mahabusu unatarajiwa kuanza kutumika baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa Karatu. Hizo ni jitihada za kuongeza kasi ya usikilizaji wa mashauri ya kesi zinazofanyika katika wilaya ya Karatu ambazo mahabusu wengi hulazimika kuwekwa kisongo na kuletwa siku ya usikilizwaji wa kesi zao.
Hayo yamesemwa na waziri wa Mambo ya ndani Mh. George Simbachawene alipotembelea eneo linalojengwa Gereza la Mahabusu huko njia panda Karatu. Amesema majengo ya sero yameshakamilika zilizobaki ni nyumba za watumishi na kujengwa uzio katika jengo la mahabusu. Mh. Simbachawene amesema amemuelekeza Mkuu wa jeshi la magereza Tanzania kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa nyumba mbili za askari pamoja na ujenzi wa uzio unakamilika ndani ya kipindi kisichopungua mwezi mmoja, ili mahabusu waanze kusikilizwa kesi zao wakiwa Karatu.
Mh. George Simbachawene akikagua jengo la magereza ya mahabusu.
Mh. Simbachawene ametembelea kituo cha polisi Karatu na kuzungumza na askari amesema mafanikio yoyote katika taifa lete; mwelekeo wa ujenzi wa viwanda, muelekeo wa ujenzi wa miundo mbinu ya msingi ya uchumi inategemea ulinzi wa jeshi la polisi. Amesema lazima askari wafanye kazi kwa kuangalia kiapo na kufanya kazi na rai wema kupata taarifa za watu wabaya.
Jeshi la polisi lifanya kazi zake vizuri amewasisitiza jeshi la polisi kusimamia haki za watu, amesema jeshi la polisi halipaswi kusimama na wahalifu au kujihusisha na kuwaonea watu. Amesema ni jukumu la askari kuhakikisha mwananchi mnyonge haki yake inalindwa. Zamani heshima ya mtu haikutokana na uwezo wake wa kifedha au cheo chake heshima ya mtu ilitokana na namna mtu anavyoishi na watu.
Mh. Simbachawene ameasa jeshi la polisi kuacha rusha na makosa yanayowapelekea kufukuzwa kazi. Amesema anajua kunachangamoto nyingi zinazokabili jeshi la polisi, amesema licha ya changamoto hizo askari waendelee kufanya kazi kwa uadilifu. Mazingira yatazidi kuwa mazuri kadri uchumi wetu unavyozidi kukua.Ulinzi na amani unategemea san
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa