Wahitimu wa Jeshi la Akiba Katika wilaya ya Karatu Mkoani Arusha wanetakiwa kuwa mstari wa mbele kuendeleza uzalendo na ukakamavu wanapotekeleza Majukumu yao ya kila siku baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa kamati ya Usalama wilaya ya Karatu Mhe. Dadi H. Kolimba akifunga Mafunzo ya Jeshi hilo la akiba ngazi ya Wilaya ambapo amewarai kuendeleza uzalendo na kukemea vitendo vyote vya kihalifu katika jamii.
Amewataka kuheshimu viapo vyao na kushiriki katika shuguli za kijamii ili jamii itambue mchango wao na kujenga imani itakayo saidia kuimarisha ushirikiano kati ya jamii na vyombo vya usalama.
Aidha amewataka kutumia ukakamavu wao kufanya kazi kwa bidii zitakazo waingizia kipato huku akiwaelekeza kuunda vikundi na kubuni miradi ili kupata mikopo kupitia Halmashauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya karatu Ndg. Juma Hokororo akizungumza katika hafla hiyo amesema Halmashauri itaendelea kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya ili kuhakikisha vijana hao wanapata kipaumbele cha ajira Halmashauri.
Amesema Halmashauri itaendelea kutenga kiasi cha fedha kupitia mapato ya ndani kila mwaka kuunga mkono kufanikisha mafunzo ya jeshi la akiba kwa kuchangia baadhi ya mahitaji Muhimu ikiwemo Sare.
Akieleza historia ya Kamandi hiyo iliyo hitimu Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Karatu SA. Komba amesema kati ya vijana 140 walioanza mafunzo hayo ni vijana 89 pekee ndio waliofanikiwa kuhitimu Mafunzo hayo wakiwemo 16 wa kike na 73 wa kiume.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa