Narrow bee fly au Nairobi fly ni aina ya wadudu ambao wako katika makundi mawili, ambayo huishi Afrika ya mashariki. Aina hizo mbili za Nairobi fly zinaitwa Paederus Eximius na Paederus Sabaeus kwa mujibu wa Wikipedia.
Wadudu aina ya Nairobi fly hushamiri sana kipindi cha mvua , ambacho mara nyingi huonekana na husambaa kwa wingi katika mazingira yetu. Katika aina hizo mbili za Nairobi fly ambazo kitaalamu (Botanic name) Paederus Eximus ni aina fupi ya Nairobi fly na Paedrus Sabaeus ni aina ndefu ya Nairobi fly.
Afisa Mhifadhi wanyamapori wilaya ya Karatu Ndg. Cornel Lengai anasema Nairobi fly ni wadudu ambao majimaji yao (Haemolymph) yana kemikali sumu inayoitwa Pederin. Anasema kamikali pederin inasumu sana endapo itagusana na ngozi ya binadamu.
Ndg.Lengai anasema wadudu hawa hawang’ati, ila mtu anapomuona mdudu anatambaa kwenye ngozi yake huamua kumpiga, au kumgandamiza juuya ngozi. Afisa Mhifandi wanyamapori Ndg. Lengai anasema unapofanya hivyo, majimaji yanayotoka kwenye mwili wa mdudu huyo baada ya kumgandamiza na akamuua ndio yanakiwango kikubwa cha kemikali sumu inayoitwa kitaalam Pederin.
Ndg. Lengai anasema kemikali hiyo inapogusana na ngozi ndio inaleta athari kama tatizo la ngozi linaloitwa (Paederu Dermatitis) Malengelenge na mara nying dalili zake hujitokeza ndani ya masaa 12-48. Ndg. Lengai anasema dalili zinazojitokeza ni kuhisi muwasho wa ngozi, kuhisi sehemu iliyoathirika na majimaji ya sumu kama panawaka moto unaoambatana na maumivu makali. Ngozi kuonekana nyekundu katika eneo liloathririka, michubuko na michirizi huonekana kama pameungua.
Ndg. Lengai anasema Jinsi ya kukinga madhara ya mdudu aina ya Nairobi fly ukimuona anatamba kwenye ngozi, ni vyema ukampuliza au kumuondoa adondoke na umuuwe kwa kitu na siyo mahusiano ya moja kwa moja na ngozi ya mwili wako (direct contact) Ndg. Lengai anashauri endapo ikitokea umemuuwa juu ya ngozi au mkononi, unashauriwa kunawa mikono haraka, kusafisha sehemu hiyo ya ngozi kwa maji mengi ya kutosha na sabauni.
Ndg. Lengai anashauri kupaka (tropical antihistamines) ambayo inaweza kupatikana kwenye dawa kama white dent ili kupunguza madhara kwenye ngozi (allegic reaction) inayotokana na sumu ya majimaji yanayotoka mwilini mwa Nairobi fly.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa