Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu, Humphrey Polepole amekagua miradi ya maendeleo mbalimbali inayosimamiwa na serikali Wilayani Karatu. Mlezi huyo wa CCM mkoa wa Arusha ameomba watendaji kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Ndugu, Polepole amesema hayo kwenye kikao kikuu cha Halmashauri ya CCM wilaya ya Karatu ,kilichofanyika leo katika viwanja vya ofisi ya CCM wilaya ya Karatu. Ndugu Polepole ametembelea mradi wa maji wa Kansay ambao Mhe.Rais Dkt, John Pombe Magufuli ametoa Million mia moja thelathini na tisa ambazo zitakamilisha mradi huo wa maji. Mradi huo wa maji ukikamilika utasaidia watu elfu nne wa kata ya Kansay. Fedha hizo zitatumika kusambaza mabomba kutoka mlimani na kuwafikia wananchi.
Ndugu Polepole amesema hata Mjini Karatu mradi wa Karuwasa unachangamoto. Mradi una pampu moja ya kusukuma maji, kwenye tanki lenye lita laki mbili na ishrini na tano. Uwezo wa pampu kusukuma maji kwenda mlimani ni lita elfu thelathini, na pampu inahitaji zaidi ya masaa saba ili kuweza kujaza tanki la maji mlimani. Dips za maji zikifunguliwa ndani masaa matatu maji yanakwisha, amesema watakaa kikao na Mkuu wa wilaya, watu wa Karuwasa, Waandisi wa Halmashauri na Uongozi wa Halmashauri ili iongezwe pampu ya pili Bwawani kwenye kisima cha pili ambacho hakifanyi kazi. Kisima kina uwezo wa kuzalisha maji mengine lita elfu ishirini na nane. Ambayo itakuwa imeongeza upatikanaji wa maji kwa asilimi mia moja.
Ndugu, Polepole amesema leo pia atakaa na wadau kwa ajili ya soko la Karatu ambalo lina upungufu wa millioni arobaini na tano kufanikisha upauzi wa soko. Amesema Karatu inatakiwa kutoa asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Mji mdogo lakini jambo hilo limekuwa likisua sua. Amesema fedha hizo za mapato ya ndani zinatumika kutoa mikopo ya kinamama na vijana na mikopo hiyo inapaswa iwe haina riba. Amesema baba akisafiri na mwanae basi baba anajukumu la kumlipia nauli mtoto.
Ndugu, Polepole ameahidi kutoa mkopo ya elimu ya juu kupitia Chama Cha Mapinduzi; kwa wanafunzi watakao maliza shule mwaka huu mwezi wa tano, na kufaulu vizuri kiwango cha daraja la kwanza, na lapili katika Shule ya sekondari Florian, ambayo ina wanafunzi wa kike tuu kidato cha tano na sita. Amesema yeye kama mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha hataki mzaha kwenye kutoa maendeleo kwa wananchi. Ndugu Polepole ameelekeza Halmashauri ya Karatu kwa miradi yote ya kimkakati ya maendeleo ambayo imekwama iletwe kwenye Chama Cha Mapinduzi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa