Sherehe za mtoto wa Afrika zimefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Endabsah. Watoto zaidi ya elfu moja walijumuika kwa pamoja na kuadhimisha siku ambayo kwa ngazi ya wilaya ilifanyika katika Tarafa ya Endabash.
Afisa ustawi wa jamii wa wilaya Abdala Nyange amesema karatu imetengeneza mabaraza ya watoto 28 yameundwa pamoja na kamati ya ulinzi wa mtoto katika vijiji 41. Karatu ina makao ya watoto 8 yanayohudumia watoto 404. Makao hayo yanawapa watoto huduma za msingi kama chakula makazi shule na malazi pamoja na mahitaji mengine ya kiutu. Ndugu Abdala amesema wilaya ya Karatu imekomesha watoto wa mtaani kwa kufanya operesheni tatu. Jumla ya watoto 89 wamerudishwa katika familia zao na wengine kuunganishwa katika elimu ya watu wazima katika kituo cha Mwema. Amesema kulikuwa kuna watoto wanaingia mtaani mchana na kulikuwa na watoto wanaingia mtaani usiku lakini hali hiyo kwa sasa haipo wilayani Karatu.
Watoto wakifurahia jambo wakati wa sherehe za siku ya mtoto wa Afrika.
Wilaya ya karatu haina tishio la watoto wa mtaani, watoto wengi wameunganisha na huduma za elimu. Ndugu Abdala amesema wananchi wameelimishwa na kupokea elimu iliyosaidia kuondoa adhaa ya watoto wa mtaani. Ndugu Abdala Nyange amesema hiyo ni hatua kubwa sana wameipiga kama wilaya.ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuwalinda watoto ili waje nao kuwalinda na kuwatunza wazazi.
Awali katika risala ya watoto iliyosomwa Monica Mrema, watoto wamempongeza Rais wa jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kutoa elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari. Watoto wameshukuru na jitihada zinazofanywa na Halmashauri kuwaondoa watoto katika ajira hatarishi na kuzuia watoto wa mitaani. Watumiwa wa ubakaji kuwajibishwa na wazazi kuwajibisha kwa kushindwa kuwapatia watoto mahitaji ya msingi.
Watoto wakiwa wamebeba bango lao katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa