Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali yamefunguliwa leo na mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Mafunzo hayo yameendeshwa na kituo cha uwekezaji kanda ya kasikazini (TIC) na yamewakutanisha wawekezaji wa sekta binafsi.
Mhe. Theresia amesema Karatu kuna wakazi 233691 na eneo la Square 3300. Karatu kuna eneo la nyanda za juu Mbulumbulu, ambalo lina mvua nyingi na wingi wa watu inakadiriwa katika km 2 unakutana na watu 74. Kuna eneo la nyanda za chini ukanda wa Mang’ola, ambalo inakadiriwa kila km 2 kuna watu 10 mpaka 7. Mh. Theresia amesema Karatu kuna taasisi za kifedha ambazo ni fursa. Amesema serikali imeanza kuandika wasifu wa mpango wa uwekezaji ambao bado upo kwenye draft.
Mh. Theresia amewapongeza Wananchi wa Karatu kwa kuwekeza sana kwenye utalii. Mhe. Theresia amesema Karatu kuna Hotel 5 zenye five stars kuna hotel zenye hadhi ya utalii 56. Kuna campsite 9 na kuna nyumba za kulala wageni 101 na kumbi nyingi za mikutano. Kuna utalii wa asili lakini bado hatujawekeza vizuri, amesema anatamani kuona watu wamewekeza kwenye banda maalum linalouza vyakula vya asili lakini pia watu watawekeze kwenye maonesho ya ngoma za asili.
Mhe. Theresia amesema kuna ardhi ya kutosha kwa wawekezaji, kuna eneo hekari zilizopimwa 84, kuna hekari 205.1 ambazo zimefanyiwa upimaji wa awali na kuna hekari 2525 ambazo hazijapimwa. Amesema kuna maeneo ya kutosha na kama eneo halijapimwa serikali itamsaidia muwekezaji kupima eneo na kupata hati. Mhe. Theresia ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza kwenye kiwanda cha Ayalabe kwa kuingia ubia na chama cha ushirika. Amesema kuna kiwanda cha G-arusha kimekamilika kimebakia kuwekwa mashine, amesema kama kuna muwekezaji atakayejitokeza serikali itatoa ushirikiano kukiendeleza kiwanda hicho. Amesema serikali inahamasisha sana uwekezaji na kituo cha umeme kinaboreshwa hivyo umeme utapatikana wa uhakika.
Meneja Tanzania investment centre (TIC) Ndugu Daudi Riganda amesema mafunzo hayo yamelenga kujenga uelewa kwa wawekezaji na wajasiriamali namna ambavyo wanaweza kusaidiwa na kituo cha uwekezaji. Amesema kituo cha uwekezaji kimelenga kuwapa uelewa wa namna ambavyo kituo cha uwekezaji kinavyoweza kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo pamoja na wafanyabishara wakubwa katika kuendeleza miradi mikubwa.
Ndugu Daudi amesema wamejikita katika kuwaeleza wajasiramali wadogo kujua kituo cha uwekezaji kinajishughulisha na kazi gani. Lakin namna ya wawekezaji wanavyoweza kunufaika na mikutano mbalimbali inayoratibiwa (TIC) ambayo inahusisha mikutano ya kwenda nje nchi au mikutano inayofanywa ndani ya nchi ikiwahusisha wafanyabiashara kutoka nje.
Ndugu Daudi amesema wajasiriamli wanatakiwa kufahamu vivutio vya uwekezaji kama misamaha ya kodi hasa katika bidhaa zinazotumika kuzalisha au mitambo.
Meneja wa SIDO mkoa wa Arusha Bi, Nina Nchimbi amesema mkutano huo umewasaidia kufahamu fursa nzuri za uwekezaji zinapotikana Karatu. Ameomba taasisi zinazoshughulika na wajasiriamali na wawekezaji ziweze kuwa na ushirikiano wa pamoja kuwasaidia wajasiriamali kutatua changamoto zao. Lakini pia taasisi hizo kuwa na ubunifu na mfumo wa aina moja wa uelewa badala kuchukua hatua kali kwa wajasiriamali na kufunga biashara zao.
Muwekezaji wa TIC Ndugu Daud RIganda akitoa presentation mbele ya wadau wa uwekezaji.
wadau wa uwekezaji wakisikiliza Mjadala mbalimbali iliyoendeshwa na kituo cha uwekezaji kanda ya kaskazini.
Wadau wa uwekezaji wakifuatilia mijadala ya kituo cha uwekezaji iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa