Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo amekabidhi pikipiki kumi na nne kwa maafisa elimu kata mbele ya ofisi za Halmashauri. Zoezi ambalo limeshuhudiwa na, mwenyekiti wa Halmashauri Mhe, Gerson Mnyenye katibu tawala wa wilaya Ndg Abbas Kayanda na Mkurugenzi mtendaji Ndg Waziri Mourice.
Mhe Theresia Mahongo amesema pikipiki walizopewa zitaongeza ari ya utendaji kazi na uwajibikaji. matarajio ni kuongeza idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka kufikia asilimia mia moja. Ni aibu kwa mwanafunzi kumaliza darasa la saba bila kujua kusoma kuandika na kuhesabu. Mkuu wa wilaya amewataka kutumia pikipiki kwa ajili ya shughuli za kazi na siyo shughuli binafsi. Mkuu huyo wa wilaya amemuomba mkurugenzi atenge gharama za matengenezo katika bajeti yake ya mwaka. Kata zilizopewa pikipiki ni Karatu, Ganako, Rhotia, Mbulumbulu, Qurus, Endamarariek, Endabash, Burger, Kansay, Oldean, Daa, Endamaghan, Mang’ola na Baray.
Mwenyekiti wa Halimashauri Mhe.Gerson Mnyenye alisisitiza maafisa elimu kata wachukue pikipiki hizo na ziwaongezee ari ya kufanya kazi kwa ufanisi. Mhe. Gerson alisema mtihani wa darasa la saba umebadilika sasa hivi wanafunzi wanamaswali ya kujieleza. Ukilinganisha na hali ilvyokuwa zamani wanafunzi walikuwa wanashedi maswali yote. Mhe mwenyekiti alimuomba mkurugenzi mtendaji kugharamia fedha za matengenezo kwa pikipiki hizo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Mkurugenzi mtendaji Ndg. Waziri Mourice katika hotuba yake ya ufunguzi alisema gharama za pikipiki hizo ni shilling za kitanzania million tisini na moja na zimenunuliwa na serikali kuu. Halmashuri imegharamia million moja na laki nne kama gharama za usafirishaji. Pikipiki hizi zinauwezo wa kutembea kilometa ishirini na tano kwa lita moja. Mkurugenzi alitoa lita tano kwa kila afisa elimu aliyepewa pikipiki na afisa elimu wa kata ya Baray yeye alipewa mafuta zaidi kutokana na umbali mrefu anaotoka.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa