Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Dadi H. Kolimba amezindua Kampeni ya upandaji miti katika shule ya msingi Simba Milima iliyoko kijiji cha Doffa kata ya Qurus. Mkuu wa wilaya ameishukuru sana wakala wa misitu Tanzania(TFS) na wadau wengine waliojitoa kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa. Wilaya ya Karatu mwaka huu inatarajia kupanda miti 2,000,000 ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chana cha Mapinduzi CCM.
Katika zoezi hilo jumla ya miti 1,000 ilipandwa ,amewataka wananchi zoezi hilo kulifanya kuwa endelevu ili kukabiliana na tabia Nchi. Pia amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ,Afisa misitu na Afisa Mazingira kuendeleza mkakati iliyokuwepo ya kuendeleza kutoa elimu ya upandaji miti kwa wananchi.
Zoezi la upandaji miti Mkuu wa Wilaya alisema litakuwa likifanyika kila baada ya miezi mitatu lengo ni kuendeleza utunzaji wa mazingira.
Mkuu wa wilaya ameutaka uongozi wa kijiji cha Doffa kutenga njia maalum ya kupitishia mifugo na kupanda miti hasa kwenye makorongo ili kuzuia mmomonyoka wa aridhi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa