Halmashauri ya Wilaya ya Karatu imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Moja kwa robo ya kwanza ya Mwaka 2024/25 makusanyo pamoja na marejesho kwa vikundi vya wanawake vijana na watu wenye ulemavu.
Takwimu hizo zimetolewa na Bi Flora Samwel Afisa Maendeleo Wilaya ya Karatu Mbele ya Mkuu wa wilaya ya Karatu wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la Utoaji mikopo kwa Vikundi vya wanawake na Watu Mwenye Ulemavu.
Dadi Horis Kolimba Mkuu wa Wilaya ya Karatu Akizindua Zoezi hilo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu kwa Kufanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha kutoka mapato ya ndani ambacho amekitaja kuwa kiasi cha kutosha kwa robo hii ya Mwaka.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kurejesha Zoezi hilo lililo sitishwa kwa maboresho ambapo amesema ni wakati wa vikundi hivyo kunufaika kupitia mradi huo wa mikopo.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Ndg Juma Hokororo amesema Kwa hatua hii ya awali wametoa Milioni mia mbili na laki tano ambapo vikundi kumi viliomba na kukidhi vigezo, vikundi tisa vilipata shilingi Milioni mia moja na Sabini na laki tano na kikundi cha vijana kimepewa shilingi milioni 30.
Hata hivyo, Vikundi vingine vinaendelea kujisajili kuomba mkopo kwajili ya kuimarisha miradi yao.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa