Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amefanya ziara katika eneo linalojengwa hopitali ya Wilayaya karatu katika kijiji cha Changarawe. Ameangalia ujenzi wa jengo la Maabara, jengo la wagonjwa wa nje na jengo la utawala.
Mhe. Mrisho Gambo ameridhishwa na hatua za ujenzi wa hospitali. Ameshukuru bodi ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kutoa shilingi million 500 kuanzisha ujenzi wa hospital. Amesema huu uwe ushuhuda kwa wananchi wa Karatu, kwamba tukipinga ujangili, tukilinda wanyamapori wetu, tukilinda hifadhi zetu faida ni kubwa sana. Hifadhi isingekuwepo watalii wasingekuja, tusingenufaika kama tunavyonufaika sasa. Ametoa wito kwa wanachi kuendelea kulinda hifadhi na kutoa taarifa ya vitendo vya ujangili kwa vyombo husika
Naye Mhifadhi wa Ngorongoro Ndugu Fredy Manongi amesema kazi iliyofanyika inawapa moyo. Ndugu Fredy anasema wao kama watu wa hifadhi walipopata ombi la fedha za awali za kujenga hospital ya wilaya walilichukulia wazo hilo kwa mtazamo chanya. Wakajenga hoja na kulipeleka wazo hilo kwenye bodi ya hifadhi ya Ngorongoro. Ndugu Fredy amesema wataomba bodi kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya hospital ya wilaya ya Karatu kwa mwaka ujao wa fedha ili iweze kukamilika. Amesema wanajua umuhimu wa karatu kwa uhifadhi lakini pia wanafahamu adhaa kubwa watu wanayopata juu ya wanayamapori. Wanyama huwa wanatoka kwenye hifadhi na wanaathiri maisha ya watu.Hivyo mamlaka ya hifadhi imeona kuna haja ya kuchangia maendeleo ya wananchi wa Karatu.
Katika taarifa ya awali injinia Venance Malamla amesema Halmashauri kwa mwaka huu wa fedha imetoa kiasi cha shilingi million 32 ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya. Mwaka ujao wa fedha Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi million 40. Wananchi wameshiriki katika ujenzi wa hospitali kwa kujitolea nguvu kazi na zoezi hilo liliisha mwezi wa nne. Mpango kazi wa sasa ambao mafundi wamesaini utadumu kwa muda wa miezi minne na utaishia mwezi wanane.
Injinia Malamla anasema mpaka sasa hatua zilizofanyika katika ujenzi wa jengo la utawala ni kusafisha eneo; kuchimba msingi, kupanga mawe kwenye msingi, kujenga tofali za msingi, kujenga zege la msingi, kupanga mawe na kusuka nondo.Kazi ya kupiga mbao kwa ajili ya ujenzi wa jamvi inaendelea ambayo kwa sasa ni 20%. Jengo la maabara; kusafisha eneo, kujenga eneo ujenzi wa mawe chini ya msingi, kujenga tofali za msingi, kujenga zege la msingi , kupanga mawe zoezi linaendelea. Jengo la wagonjwa wa nje: kusafisha eneo, kuchimba msingi kupanga mawe, kujenga mawe chini ya msingi na kusuka nondo kazi bado inaendelea. Injinia Malamla amesema mpaka sasa imetumika million 249339475. Injinia Malamla amesema million 22000,194, ununuzi wa vifaa vya ujenzi million 222717475 na mafuta million 4428000 elfu.
Injinia Malamla amesema wanapata changamoto kipindi hiki cha mvua kupeleka vifaa vya ujenzi eneo la mradi. Magari ya mawe, mchanga, na kokoto kushindwa kufika eneo la ujenzi. Kazi za ufundi kukwama kwa sababu ya mvua kunyesha, hivyo wameamua kutumia mda mchache mvua inapopungua kwa wazabuni kuleta vifaa eneo la ujenzi na mafundi kutumia mda mchache wakati mvua inapopungua kuendelea na ujenzi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa