Uongozi wa Halmashauri ya kijiji cha Qaru uliomaliza muda wake umekabidhi nyaraka na Mali za kijiji kwa uongozi ulioingia madarakani.Makabidhiano yamefanyika katika ukumbi wa ofisi ya kijiji cha Qaru na kuhudhuriwa na wajumbe wa kijiji ambao wamejiridhisha kwa kuona maeneo ya kijiji na vifaa vilivyokabidhiwa.
Afisa tarafa wa tarafa ya Endabash Bi, Leina Swale amepongeza uongozi wa kijiji uliomaliza muda wao wa uongozi na amepongeza serikali iliyoingia madarakani. Amesema kijiji cha Qaru kimekuwa na shida ya kugawanya makabidhiano ya mali. Kuna mali zimetengwa kuwa za Mweneyekiti wa kijiji na mali nyingine zimetengwa kuwa za Mtendaji wa kijiji. Bi Leina amesema mali zote za kijiji zinapaswa kutunzwa na Mtendaji wa kijiji na zitasimamiwa na Mwenyekiti wa kijiji ameelekeza uongozi huo mpya upokee maelekezo hayo. Amesema ni haki ya wanakijiji wote kujua mali za kijiji amesema ni vizuri kila mwaka uongozi wa kijiji ukapitia orodha ya mali (review) zote za kijiji kujiridhisha.
Afisa tarafa Bi, Leina Swale (katikati) akimsikiliza Mwenyekiti wa zamani ndugu Richard Dawte akielekeza mipaka ya maeneo yanayomilikiwa na kijiji cha Qaru.
Afisa tarafa Bi, Leina ameelekeza viongozi wa kijiji kuwa wawazi katika uongozi wao, amesema kijiji cha Qaru kuna matatizo ya migogoro ya ardhi. Upimaji wa ardhi kupanga matumizi bora ya ardhi utafanyika amesema kabla zoezi hilo kufanyika ni vyema viongozi waliopewa dhamana ya uongozi wa kijiji cha Qaru kufanya upembuzi yakinifu kwenye maeneo yenye matatizo ya ardhi ili kujiridhisha na kuondoa migogoro ya ardhi.
Bi. Leina ametoa maelekezo juu ya ujenzi wa zahanati Durgeda, amesema usimamizi wa ujenzi utasimamiwa na serikali ya kijiji cha Qaru. Bi Leina amesisitiza hata ikitokea kwenye maelewano kitongoji cha Durgeda ikapata uongozi wa muda kwa kadri ya maridhiano yatakavyokuwa, kitongoji kile bado kipo katika usimamizi wa serikali ya kijiji cha Qaru. Bi, Leina amesema kwenye makabidhiano kuna miradi viporo ya maabara, zahanati, na na ujenzi wa ofisi iliyokabidhiwa kwa uongozi mpya. Ametoa maelekezo kwa uongozi wa serikali ya kijiji kujikita kusimamia na kumaliza miradi viporo. Bi, Leina amesema kuna ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili shule ya sekondari Qaru, na nilazima watoto wote waende shule. Amehimiza uongozi wa serikali ya kijiji kuweka mikakati ya kujenga madarasa hayo, amesema Mkuu wa mkoa wa arusha Mhe. Mrisho Gambo atapitia kukagua hatua za ujenzi kwa shule zenye uhaba wa madarasa.
Ndugu Richard Dawte Mwenyekiti aliyemaliza muda wake akinyoosha mkono kuonesha mipaka ya eneo la uwanja wa mpira wa Miguu zamani linalomilikiwa na kijiji cha Qaru.
Bi Leina amehimiza uongozi wa kijiji cha Qaru kusoma mapato na matumizi kwa wakati, amesema itasaidia kuondoa mashaka. Amempa maelekezo mtendaji wa kijiji, fedha yeyote inayokusanywa kwenye Mamlaka ya kijiji ipelekwe Benki. Bi Leina amesisitiza kwa watendaji wa kijiji kutotumia fedha zilizokusanywa kabla ya kuwekwa Benki (fedha mbichi), amesema lazima fedha ziwekwe banki halafu zifanyiwe bajeti na serikali ya kijiji.
Afisa Mtendaji wa Kata ndugu Joseph Ezekiel amesema kamati ya ardhi na mazingira ipime maeneo ya wazi ijiridhishe. Amesema kuna bati ambazo zilikuwa ni zamradi wa zahanati Durgeda ambazo zimeazimwa, mtendaji wa kata ametoa malekezo kwa uongozi wa kijiji kusimamia urejeshwaji wa batI hizo ili zitumike kwenye mradi husika.
Ndugu Ezekiel amesema kuna mashine ya kijiji ipo kwenye ofisi ya chama amesema mashine hiyo irudishwe ofisi ya kijiji. Kuna eneo la mkondo wa maji uliopo kwenye mpaka wa kijiji cha Qaru na Endabash ambalo lilishughulikiwa na maji yakaanza kupita, amesema sasa watu wameenda kupanda migomba katika eneo hilo na kusababisha maji kuanza kutuwama tena kwenye eneo hilo ametoa maelekezo kwa uongozi wa Halmashauri ya kijiji kufungua mkondo huo wa maji.
Awali Mtendaji wa kijiji Bi, Janeth Mollel alisema vitu alivyokabidhiwa ni Faili la mikataba, Faili la Tassaf, amekabidhiwa bati za Gurgeda 64 na amesema inasemekana bati zilikuwa 72 awali. Amekabidhiwa trekta, boza moja, trela la trekta, reja mbili moja imetumika na moja inaendelea kutumika. Amekabidhiwa jengo la Godauni, kabati za ofisi, safe ya kijiji, mashine mbovu, meza mbili, kiti kimoja benchi nane, hati ya Kinihhee, hati ya Halmashauri ya kijiji, kadi ya trekta, kitabu cha wageni, faili la kitabu cha wageni, faili la Halmashauri ya kijiji, vifaa vya world vision, net zilizohifadhiwa Godauni, kuna bati chakavu, kuna baiskeli tatu zipo Godauni, Mizani, kuna nyavu zilizowekwa Godauni, kuna dramu kuna madumu na mafaili.
Naye Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Ndugu Richard Dawte akitoa tarifa yake ya makabidhiano amesema kijiji cha Qaru kina shule mbili za msingi na sekondari moja. Amesema kijiji kina shamba la la heka kumi na robotatu, ina mizani ya duka ambayo ni mbovu, kombe la mchezo, kuna safe mbovu ya pesa, kiwanja heka moja chenye miti, kuna mabomba krash, sanduku la huduma ya kwanza, kuna kadi ya zamani huduma za benk kuna, taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi wa tisa ambayo haijasomwa, uwanja M 19 kwa 30, kuna uwanja wa SM 15 kwa SM 30 kuna eneo la uwanja robo, juu ya eneo la uwanja ulipokuwa uwanja wa mpira wa miguu, kuna eneo la uwazi kwenye sehemu ya kitongoji cha krash, kuna eneo wazi linalopakana na eneo la chama cha mapinduzi, kijiji kina viwanja viwili vya mpira, uwanja wa zamani na uwanja mpya wa mpira unaomilikiwa na serikali za kijiji, maeneo yote yapo katikati ya kijiji cha Qaru. Huduma za maji kuna dp 20 za umma na mbili za taasisi moja ya sekondari na moja ya shule ya msingi. Majengo ya kijiji, kuna jengo la Ofisi ya kijiji, kuna jengo la Godauni, kuna hati ya mitambo ya mawasiliano.
Mwenyekiti anayeingia madarakani Ndugu Justin Sulle na wajumbe wa kikao hicho walikubaliana taarifa hizo ziunganishwe na iwe taarifa moja. Baada ya kutembelea na kuona vitu vilivyosomwa na Mtendaji wa kijiji pamoja na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake. Katika mkutano huo wa makabidhiano wajumbe waliazimia taarifa iwe inaandikwa moja kuanzia sasa na nakala apewe Mtendaji wa kijiji na nakala nyingine apewa mwenyekiti wa kijiji.
Wajumbe wapya wa serikali ya kijiji wakikakugua vitu vilivyokabidhiwa na uongozi wa kijiji cha Qaru uliomaliza muda wake.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa