Watendaji wa serikali mnapaswa kuhakikisha mnawaelimisha wananchi wanaohitaji kupata ardhi ili wafuate taratibu zote za kupata ardhi katika eneo husika. Kushindwa kufuata taratibu za kupata ardhi kunasababisha migogoro ya ardhi ambayo hujitokeza baada ya kutokuelewana.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh, Abbas Kayanda alipokuwa akizungumza na wananchi katika kitongoji cha Manusay katika kijiji cha Endala. Amemuelekeza Mtendaji wa kijiji cha Endala kuhakikisha anasimamia kikamilifu ndani ya siku thelathini madai ya Bi, Benedeta Karama aliyedai eneo lake limetwaliwa kwa nguvu. Amesema lazima tusimamie misingi ya haki na tufuate taratibu na miongozo katika utendaji wa shughuli za serikali.
Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Manusay
Mh. Kayanda amemuelekeza Afisa tarafa wa tarafa ya Endabash Bi, Leina Swale kusimamia na kutatua mkwamo wa upatikanaji wa maji katika kijiji cha Endala, kijiji kiliingia makubaliano na Tyrilin safari lodge kwa masharti ya kuwasaidia kupata dp mbili za maji.
Kuhusu baraba Mh. Kayanda amesema barabara ya Endala ipo kwenye mpango wa ukarabati wa Tarura. Amesema mwaka huu wa fedha daraja moja linajengwa na bajeti ya mwaka ujao wa fedha kuna daraja jingine ambalo limeingizwa kwenye bajeti. Serikali inaendelea kutambua umuhimu wa barabara ya endala kwa sababu inaunganisha Endala na meneo mengine ya wilaya ya Karatu.
Katika hatua nyingine Mh. Abbas Kayanda ametembelea eneo la linalodaiwa kuwa linapatikana madini ya dhahabu katika kijiji cha Endala. Mh. Kayanda ameelekeza uongozi wa serikali ya kijiji kusimamia taratibu ili kila mwenye uhitaji wa kujishughulisha uchimbaji wa madini aweze kupata leseni inayomuwezesha kujishughulisha na uchimbaji wa madini. Amesema ni vyema serikali ya kijiji itoe elimu ya kwa wachimbaji wadogo wadogo juu ya umuhimu wa kuwa na leseni.
Mh. Abbas Kayanda akizungumza katika eneo la machimbo katika kijiji cha Endala.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Endala Ndg. Thomas Dawite amemshukuru Mkuu wa wilaya kwa ziara aliyofanya katika eneo hilo la machimbo madogo madogo. Amesema wao kama Halmashauri ya kijiji walikuwa wanafurahia fedha ya ushuru waliokuwa wakipata katika machimbo hayo. Amesema sasa watasimamia na kuhakikisha kila mchimabaji anapata leseni ya uchimbaji wa madini.
Ameongeza kusema taratibu zilizowekwa na serikali juu ya ukataji wa leseni zinasaidia wachimbaji kutojiingiza na uchimbaji wa madini kiholela. Amesema utaratibu huo utasaidia pia katika utunzaji wa mazingira kwa sababu hakuna wachimbaji watakaojihusisha na uchimbaji wa madini kiholela bila kujiridhisha upatikanaji wake.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa