Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Luteni Josephine Paul Mwambashi ametembelea mradi wa vijana wa kikundi cha amani wanaojihusisha na utengenezaji wa maandazi. Luteni Mwambashi amewapongeza vijana kwa kufanya kazi halali za kuwaingizia vipato. Amewahimiza kuhakikisha wanafuata miongozo ya biashara na kuzingatia kanuni na taratibu za afya.
Kikundi cha amani wanaojihusisha na utengenezaji wa maandazi. mradi wa uzalishaji maandazi wa kikundi cha vijana cha Amani unauwezo wa kuzalisha maandazi kati ya 700 hadi 1000 kwa siku. Wanatarjia kuzalisha mikate 300 kwa siku, kwa kupitia mradi huo wameweza kuajiri vijana wanne, ambao wawili wako jikoni na wawili wanasambaza bidhaa za kikundi.
kikundi hiki cha Amani NMC Karatu kilianza rasmi Novemba mwaka 2020 kikiwa na vijana 10 kwa mtaji wa Tshs 7,770,000/= na baadae Halmashauri ikawakopesha Mkopo usio na riba wa Tshs 4,000,000/=. Lengo la Kikundi cha amani ni kufanya biashara ya utengenezaji wa maandazi na uokaji wa mikate ili kujiendeleza Kiuchumi na kutoa huduma kwa jamii inayozunguka.
Matukio katika picha kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru alipotembelea kikundi cha vijana cha Amani NMC
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa