Siku ya mazingira imeadhimishwa wilayani Karatu, kwa wadau wa siku ya mazingira kuokota taka pembezoni mwa barabara kuu. Zoezi la kuokota taka limeanza geti la Ngorongoro mpaka geti la Manyara likiongozwa na Afisa Mazingira ndugu Gadiye John.
Siku hii ya kilele cha juma la mazingira imeambatana na sikukuu ya Iddi pamoja na hali ya baridi kali na manyunyu hali iliyosababisha umande. Upekee wa siku hii ni namna Afisa mazingira alivyohamasisha kwa gari la matangazo, lakini pia kutumia usafiri binafsi kusomba taka na kuungwa mkono na wadau wa mazingira. Madhari ya barabara yalivyobadilika baada ya kufanya usafi wa kuondoa uchafu.
Ndugu Gadiye amesema leo ni kilele cha juma la wiki ya mazingira. Tumeamua kuanza kufanya usafi kuanzia lango la mamlaka ya Ngorongoro kuelekea lango la mamlaka ya hifadhi ya ziwa Manyara. Amesema changamoto za mazingira ni kubwa ndio maana watu wamejitokeza, wadau walioalikwa ni theleathini na saba ambao ni hotel mbalimbali za kitalii lakini pia mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na mamlaka ya hifadhi ya ziwa Manyara. Amesema eneo lilofanyiwa usafi wa mazingira ni takribani km 35.
Ndugu Gadiye amesema wamehamasisha wananchi kwa kupitisha gari la matangazo juu ya kilele cha juma la Mazingira. Lakini pia kuhamasisha watu kuacha kutumia mifuko ya plastiki na wamehamasika kufanya usafi katika maeneo yao ya makazi. Amesema mwananchi akivunja sheria ya utunzaji mazingira sheria ziko wazi kwa sababu elimu imetolewa kuanzia ngazi ya kitongoji hadi eneo la katikati ya mji. Sheria zinazotumika ni sheria ya uhifadhi Mazingira ya mwaka 2004. Kuna sheria ndogo ya wilaya ya Karatu ya uhifadhi wa mazingira ambazo mtuhumiwa akipatikana na hatia anaweza kutozwa kiasi cha 50000 kama adhabu au kifungo cha miezi mitatu mpaka sita.
Ndugu Gadiye amesema zoezi la uhifadhi wa mazingira ni endelevu ndio maana hata taka zilizokusanywa ni kiasi kidogo. lakini pia upo mpango wa kuweka alama za kukataza kutupa taka hovyo sehemu mablimbali za mji lakini pia kutengeneza tangazo litakalokaa kwenye madirisha ya magari. Lengo ni kutoa uelewa mkubwa wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na kuacha kutelekeza taka hovyo.
Wadau wakiotoka taka pembezoni wa barabara licha ya hali ya baridi kali.
Wadau wakiendelea na zoezi la kuokota taka katika barabara kuu wilayani Karatu.
Wadau wakikusanya taka na kuweka kwenye gari tayari kwenda kutupwa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa