Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi imetembelea jengo la zahanati kijiji cha Kainam Rhotia kujionea hali ya ujenzi wa jengo la zahanati. Jengo hilo la zahanati lililoanza kujengwa takriban miaka kumi na mbili iliyopita bado liko katika hatua ya umaliziaji.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ndugu Lucian Akonnay amesema lengo la ziara yao ni kuona sera zao za chama zinatekelezwa kwa vitendo. Amesema wameona jengo la zahanati hiyo limekwama muda mrefu jambo linaloleta adhaa kwa wananchi kutembea umbali wa km 7 kufuata matibabu kijiji cha Rhotia kati.
Ndugu Waziri Mourice amesema Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi million 10 katika kukamilisha ujenzi wa zahanati. Amesema kulikuwa kuna shida ya kupanga bajeti miaka ya nyuma kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo kijiji cha Kainam Rhotia. Ndugu Waziri Mourice amesema watatumia vifaa vilivyobakia kuweka madirisha na kuweka sakafu katika jengo la zahanati. Ujenzi wa ukamilishaji wa jengo la zahanati, utaanza mapema kabla ya robo ya pili ya mwaka haijaanza.
Katika taarifa hiyo afisa mtendaji Nyakangara Mbogo amesema ili jengo hilo limalizwe na kutumika linahitaji kiasi cha shilingi million 52 na laki tano. Jengo lina ukubwa wa vyumba 16 katika ujenzi huo Halmashauri ilitoa kiasi cha shilingi million 28 na wananchi walishiriki kukusanya mawe kuchimba msingi na kugonga kokoto. Ndugu Mbogo amesema vifaa vilivyobaki na vinavyotarajiwa kutumika kumalizia ujenzi wa zahanati ni bati 49 geji 28, mbao 120 grill za madirisha zipo 16 vifaa hivyo vipo kwenye ofisi ya kijiji. Ofisi ya kijiji imeandaa mkakati wa kushirikisha wanakijiji kuchangia mwaka huu wa fedha kiasi cha shilling cha elfu 20 kuchangia ujenzi wa zahanati, kijiji kina kaya 670 hivyo kutarajia kukusanya kiasi cha fedha Million 13 na lakin nne.
Benadicto John mkazi wa Kainam Rhotia anasema wanapata adhaa kubwa ya kupata huduma za afya. Ameiomba serikali kuharakisha kukamilishwa ujenzi wa jengo la zahanati katika kijiji hicho. Amesema wakinama wajawazito wanaathrika zaidi kwa umbali wanaotembea kupata huduma za afya na mara nyingine kupoteza maisha.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa