Afisa mwandikishaji jimbo la Karatu ndugu Waziri Mourice amefanya ziara katika vituo vya uandikishaji daftari la maboresho la kura Tarafa ya Mbulumbulu. Katika ziara hiyo ameambatana na Afisa wa tume ya uchaguzi pamoja na Afisa Tehama wilaya.
Ziara hiyo ililenga kuangalia utendaji wa Maafisa wandikishaji na wataalamu wa BVR KIT katika kutekeleza majukumu yao katika siku ya kwanza ya uandikishaji kati ya siku sita zilizobakia. Zoezi hili la uandikishaji linafanyika Wilaya ya Karatu sasa na tume ya taifa ya uchaguzi imetoa maelekezo kupitia vyombo vya habari hakuna mda utakaongezwa baada ya muda elekezi kuisha. Afisa Mwandikishaji ndugu Waziri Mourice ametembelea vituo 34 kati ya vituo 46 alivyojipangia kutembelea tarafa ya Mbulumbulu. Lengo ni kujionea mwenyewe hali ya zoezi badala ya kusubiri taarifa kutoka kwa wataalamu. Amewahimiza watendaji kuwa makini katika uandikishaji na kuhifadhi kazi data za kila siku (Back Up) ambayo ni muhimu kupata idadi ya watu walioandikishwa kila siku. Amestaajabishwa baadhi ya vituo kukosa mawakala wa vyama wanaoangalia mwenendo wa zoezi hilo.
Afisa Mwandikishaji akiangalia utendaji wa maafisa waanikishaji moja ya kituo Tarafa Ya Mbulumbulu.
Ziara hiyo imesaidia pia kurekebisha dosari za kitaalamu zilizokuwa zinajitokeza kwa waandikishaji katika vituo vyao. Dosari zilizobainika kubwa katika ziara hiyo ni baadhi ya waandikishaji kutotumia waya (cable) husika katika baadhi ya vifaa. Jambo lilokuwa linasababisha BVR KIT kutoingiza umeme unaozalishwa kwa njia ya jua. Baadhi ya waandishi kusahau kuunganisha vifaa vya umeme jua ambavyo ni muhimu katika zoezi la uandikishaji. waandikishaji wengine kugeuza kadi za kupiga kura wakati wa kuzitengeneza. Maafisa hao walioambatana na mkurugenzi waliweza kutatua matatizo hayo na kutoa malekezo ya kina. Ndugu Waziri ameweza kutambua vituo ambavyo vinahitaji genereta kwa ajili ya kuchaji vifaa hivyo ili viweze kuendelea kufanya kazi.
Ndugu waziri amewaelekeza Maafisa waandikishaji kuweka matangazo ya vituo barabarani ili kuonesha eneo la kujiandikishia. Ametoa maelekezo hayo baaada ya kupita baadhi ya vituo bila kuona mabango yanayoenesha sehemu za kujiandikishia wapiga kura njiani badala yake wameweka bango kituoni tuu. Amehimiza watendaji katika maeneo yao ya kazi kufanya mikutano ya kuhamasisha watu kujitokeza kwa ajili ya kuboresha daftari la wapiga kura. Sambamba na hilo Ndugu Waziri Mourice ameweka magari ya matangazo yanayotangaza maeneo mbalimbali kuhamasisha watu kujitokeza. Amesema lengo la kufanya hivyo ni ili Karatu ifanye vizuri katika zoezi la uandikishaji.
Ndugu waziri ametumia ziara hiyo kuwakumbusha waandikishaji namna ya kutumia fomu namba mbili ambayo inajaza taaarifa mbalimbali za uandikishaji kwa siku. Amehimiza waandikishaji kuwaelekeza wananchi hasa wale waliopoteza kadi zao za kupiga kura kuja na nakala ya polisi inayoonesha upotevu wa kadi zao au kuja na barua ya utambulisho kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji inayoonesha upotevu wa kadi ili mwananchi aweze kuandikwa na kupatiwa kadi mpya.
Afisa Mwandikishaji Ndugu Waziri Mourice akiweka kitambaa maalumu kwa ajili ya kupiga picha za waandikishwaji moja ya kituo Tarafa ya Mbulumbulu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa