NA TEGEMEO KASTUS
Wananchi wanaolima ndani ya mita 60 kwenye chanzo cha maji, wamepewa muda wa kuondoka kwa hiari yao wenyewe. Ili kuendelea kulinda vyanzo vya maji kwa kizazi cha sasa na kizazi cha baadae. Kuhifadhi vyanzo cha maji ni jambo la kisheria.
Hayo yamesema na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara Mbuganyekundu. Amesema awali wananchi wanaojihusisha na kilimo kwenye vyanzo vya maji ambavyo viliwekewa mipaka (becon) mwezi wa pili na zoezi hilo kuzinduliwa na mkuu wa mkoa, walikaa kwenye mikutano na kukubaliana mwisho wa kulima ni mwezi wa saba tarehe 12 mwaka huu. Mh. Kayanda ameagiza mpaka kufika siku ya jumatatu wawe wameondoka wenyewe kwenye maeneo hayo kwa hiari yao.
Mh. Abbas Kayanda katika matukio tofauti wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Mbuga nyekundu Mang'ola.
Mh. Kayanda amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi kufanya fujo pindi changamoto kwenye mikondo ya umwagiliaji inapotokea. Amesema wananchi wanapaswa kufuata utaratibu wa kuwasilisha malalamiko nasikujikusanya na kufanya fujo. Amesema mkiwakilisha changamoto kwa uongozi wa mikondo ya umwagiliaji watawasIlisha kwenye uongozi wa Jumuiya ya watumia maji bonde dogo la Eyasi (JUWAMABOE) na wataitatua.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akizungumza wananchi wakati wa mkutano wa hadhara Mbuganyekundu Mang'ola.
Mh. Kayanda ameelekeza uongozi wote wa JUWAMABOE kukaa kikao na kutatua tatizo la umwagiliaji masaa tisa ambalo linalamikiwa na watumiaji mikondo ya umwagiliaji maji Mbuga nyekundu. Amesema ni vyema Juwamaboe kukaa na kutumia busara katika kutatua mvutano huo wa masaa tisa ya umwagiliaji.
katika mkutano huo Mh. Kayanda amegusia swala la kuchangia maendeleo amesema lazima wananchi wajitolee kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo. Kuna michango ya ujenzi wa maabara kituo cha mbuga nyekundu na kijiji kinadaiwa kuchangia million 13 na hazijatolewa. Amesema katika ujenzi wa bweni shule ya sekondari Baray, kijiji cha Mbuga nyekundu kinadaiwa million 6. Miradi hii ni ya kwetu sisi sote
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa