Wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na wananchi wilaya Karatu leo wameungana na ziongozi wa wilaya kupanda Miche ya miti katika eneo la hospitali ya wilaya kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika.
Zoezi hilo limeongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Mhe: Dadi Kolimba pamoja na mkurugenzi wa halmashauri Ndugu Karia Magaro limehudhuriwa pia na watumishi wa halmashauri ambapo waliweza kupanda Miche ya miti zaidi ya 500 katika eneo la hospitali hiyo.
Akizungumza na wananchi na wadau mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kuwa wazalendo katika katika kuyaenzi viongozi waliopigania Uhuru nchi hii.
Alimwagiza mkurugenzi kuhakikisha mazingira ya hospitali hiyo yanakuwa na muonekano mzuri kwa kutunza miti waliyopanda leo kwani Ni Jambo la kujivunia wilaya kuwa na hospitali ya wilaya ambapo tangu kuanzishwa kwake haikuwa na hospitali.
"Mkurugenzi nakuagiza hakikisha Miti tuliyopanda Leo ya kivuli na matunda inakuwa na uangalizi mzuri wa kukua ili kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi , pia itakuwa na faida ya kupata matunda."alisema Kolimba.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmshauri hiyo Karia Magaro aliwashukuru wananchi pamoja na wadau walioshiriki katika zoezi hilo ambapo aliwahakikishia Miche hiyo inakua na mandhari mazuri ya hospitali hiyo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa