Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu ndugu Waziri Mourice amekutana na watendaji wa kata katika ukumbi wa Halmashauri. Katika kikao chao cha ndani Mkurugenzi amezungumzia uteuzi wao kama waandikishaji wasaidizi wa zoezi la undikishaji na uboreshaji dafatari la wapiga kura.
Zoezi hilo linatarajiwa kuanza kwa kanda ya kaskazini ikijumuisha na mkoa wa arusha tarehe 18 mwezi wa saba. Uandikishaji utafanyika kwa siku saba na matangazo ya kuomba nafasi hizo tayari yameshatoka na kuwekwa kwenye mbao za matangazo. Taaarifa hizo pia zimesambazwa na watendaji kata ambao watazibandika kwenye mbao za matangzo ili kufikisha taarifa kwa kila mwananchi.
Ndugu Waziri Mourice amesema kwenye kikao hicho yeye ni Mkurugenzi wa Halmashauri wilaya ya Karatu na ni Afisa muandikishaji katika uboreshaji wa daftrari la wapiga kura wilayani Karatu. Amesema ameteuliwa na mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi tarehe 26/6/219 kuwa afisa muandikishaji na alitakiwa kuteuwa watu wa kumsaidia ambao ni watendaji kata. amesema kutakuwa na nafasi za wataalamu watakao omba kushiriki katika zoezi na tayari tumeshabainisha sifa zinazotakiwa. Watendaji kata walioteuliwa watakuwa maafisa waandikishaji wasaidizi katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura. Wanapaswa kuzingatia sifa za muandikishaji ambazo nimewasisitiza kuzifuata. Amesema afisa atakaye kwenda kinyume na maelekezo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Sifa ya muandikishwaji ni mtu aliyetimiza umri wa miaka 18.
Maafisa waandikishaji wakiwa katika kikao chao
Ndugu Waziri Mourice amesema watendaji kata wameteuliwa kwa sababu ndio wasimamizi wa shughuli zote za kata katika kata. Mtendaji wa kata ndiye mlinzi wa usalama na amani hivyo ni sahihi kwa wao kusimamia zoezi hilo. Watendaji wa kata wamepata barua za uteuzi wa kuwa maafisa wasaidizi wa uandikishaji kuanzia tarehe 1/7/2109. Amesema kikao cha leo kilenga kuwakumbusha majukumu yao kama maafisa waandikishaji wasaidizi, katika kuhakikisha wanafuata vigezo vya uandikishaji. Amesema moja ya kigezo cha uandikishaji ni raia anayeandikishwa lazima awe ni mtanzania. Amesema anayeandikishwa lazima awe na sifa ya umri ambayo ni kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Maafisa waandikishaji wasaidizi wakisikiliza jambo kwa afisa mwandikishaji wa wilaya
Ndugu Waziri Mourice amesema baada ya kupata watu watakaofanya kazi za uandikishaji kwa nafasi zilizotajwa watapata semina ya siku mbili. Amesema katika ngazi ya wilaya afisa muandikishaji ana watu wanne ambao watakuwa wanapita katika kila kituo kujionea maendeleo ya kazi. Maafisa wasaidizi wa uandikishaji ngazi ya kata, wamepewa mafuta lita kumi pamoja na rimu za makaratasi kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya kutekeleza shughuli za uandikishaji.
Maafisa wasaidizi na waandikishaji wa daftari la uboreshaji wapiga kura wakifutilia kwa makini maelekezo kwenye kikao.
Peter Ngumuo kaimu afisa Uchaguzi amesema maafisa wasaidizi wamepewa nasaha namna ya kutekeleza kazi zao kwa ufasaha. Amesema afisa Mwandikishaji wilaya amewapa maagizo ya kutembelea vituo vya uandikishaji na kutoa taarifa kwa Afisa muandikishaji ngazi ya wilaya. Amesema kikao hicho ni muhimu kwa maafisa wasaidizi wa uboreshaji daftari la wapiga kura ili wasije wakajisahau katika utekelezaji wa shughuli zao. Kaimu afisa uchaguzi amesema kikao hicho kimelenga kuwapa matangazo ya nafasi za uandikishaji ili Mafisa hao wasaidizi wapeleke matangazo ya nafasi hizo za kazi ngazi ya kata.
Maafisa wakiweka mafuta tayari kwa kuanza kuanza majukumu ya kazi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa