Semina ya wataalamu wa BVR na Maafisa wasaidizi waandikishaji imefanyika katika ukumbi wa Karatu sekondari. Semina hiyo ya siku mbili imelenga kuwajengea uwezo maafisa waandikishaji wasaidizi utayari wa kufanya maboresho ya daftari la mpiga kura, zoezi linategemea kuanza siku chache zijazo 18/7/2019.
Mgeni rasmi wa mafunzo hayo Ndugu Abbas Kayanda katibu tawala wa wilaya ya Karatu; alyefungua semina hiyo, amesema zoezi hilo ni muhimu sana kwa wataalamu wa BVR na maafisa wasaidizi. Tunataka wilaya ya Karatu iwe wilaya ya kwanza kufanya vizuri katika zoezi la uandikishaji kwa mkoa wa arusha. Amesema atakuwa anapita katika maeneo mbalimbali ya vituo kujionea utekelezaji wa zoezi hilo. Tusikubali kushindwa na wilaya nyingine, kwa sababu tumefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi hili.
Picha ni wataalamu wanaotarajiwa kufanya zoezi la BVR wakiskiliza hotuba ya mgeni rasmi.
Ndugu Kayanda amewaasa waandikishaji juu ya kutunza vifaa hivyo, amesema kupewa mashine ni kupewa dhamana. Tukiharibu mashine hizi inatia doa kwa sababu zinategemewa kutumika sehemu nyingine baada ya zoezi kumalizika Karatu. Hifadhi mashine sehemu salama, kwa sababu chochote kikitokea cha uharibifu kwenye mashine ya BVR KIT utawajibishwa. Amesema si vyema kuwajibishana kwa vitu visivyo na msingi sana. Nimatumaini yetu kwamba vifaa hivyo vitatunzwa ili viende vikatumike sehemu nyingine.
Ndugu Kayanda amehimiza ushirikiano katika utendaji kazi wa zoezi la maboresho ya daftari la wapiga kura. Amesema tusiende tukaanza kutunishiana misuli kuonesha nani ni mkubwa katika kazi tunayoenda kufanya, siyo lengo la kazi hii. Amesema bila ushirikiano hatuwezi kufanya vizuri wenyewe, na busara lazima itumike wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo. Amesema katika zoezi hilo kutakuwa na mawakala wa vyama vya siasa; ambao wanaruhusiwa kuwepo ili kuona zoezi hili namna gani linavyoenda, amewaomba wataalamu hao kuwapa ushirikiano. Amesema wapeni ushirikiano ili waone namna gani zoezi hili linafanyika katika hali ya uwazi. Amesema mawakala wa siasa hawaruhusiwi kuingilia kazi ambazo mnazifanya, wala kukupangia kitu unachopaswa kukifanya. Wapo mawakala wa vyama vya siasa huwa wanajifanya wanajua zaidi kuliko wewe uliyepewa kazi hiyo. Amesema mawakala wa siasa wanapaswa kusema, kama kuna shida yeyote ili aweze kusaidiwa lakini si kuingilia utaratibu unaofanywa katika uandikishaji.
Moja ya mwandikishaji akitafakari jambo
Ndugu Kayanda amesema katika utekelezaji wa zoezi hilo la maboresho ya daftari la mpiga kura, amewaasa watendaji hao kutoa vipaombele kwa wagonjwa, wazee, kinamama wajawazito, na walemavu. Amehimiza busara kutumika katika zoezi hilo kwa sababu linahusu mstakabali wa watu katika upande wa demokrasia. Uzoefu unaonesha katika kazi hizi hasa siku za mwanzo, watu huwa hawajitokezi wengi, lakini hiyo siyo sababu ya kufunga kituo lazima tufanye kazi kwa kuzingatia maelekezo.
Afisa Mwandikishaji Ndugu Waziri Mourice amesema kuna ziada ya watu 4 kila kata, ili dharura ikitokea kwa mmoja wa waandikishaji nafasi iliyoachwa wazi ijazwe na waandikishaji hao wa ziada. amesema kutakuwa na watu wa BVR KIT 56 na waandikishaji wasaidizi 56. Maafisa hao wamehudhuriwa mafunzo hayo ya Maafisa waandikishahji na kuapishwa kiapo cha kutunza siri na kiapo cha kutokuwa mwanachama wa kisiasa. Amesema kufanya hivyo kuna wafanya waandikishaji kuwa huru kufanya shughuli za serikali kwa uhuru bila mfungamano na chama cha siasa. Ndugu Waziri Mourice amesema wataalamu wa BVR KIT na Maafisa waandikishaji watakaojihusisha na zoezi hilo ni 556 ukijumlisha na wale maafisa wa ziada.
Umakini wa kusikiliza wakati mgeni rasmi anazungumza.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa