Na Tegemeo Kastus
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Technolojia Dk. Avemaria Semakafu amefanya ziara ya siku moja wilaya ya Karatu. Katika ziara hiyo Naibu katibu mkuu amekabidhi vijana ishirini kutoka Karatu katika chuo cha maendeleo ya jamii kilichopo Mto wa mbu wilaya ya Monduli.
Naibu katibu mkuu wa wizara Dk. Semakafu amelipongeza shirika la world eduaction initiative (WEI) kwa mradi wa kuwapa elimu mbadala mabinti waliokosa elimu. amesema tatizo hilo linaathiri sana kaya masikini. Wizara ya elimu imepanga kuwasaidia mabinti waliokosa elimu kupitia program ya elimu haina mwisho. Amesema namna anavyoathirika mtoto wa kike na anavyoathirirka mtoto wa kiume ni tofauti. Mtoto wa kiume akiacha masomo utamkuta ameajiriwa na anafanya kazi kama muuza duka, vibanda vya nyama choma au muongoza utalii. Mtoto wa kike akikosa elimu atafanya kazi zisizo na staha amesema utamkuta ameajiriwa kama mhudumu wa baa, amekuwa mhudumu wa ndani, au utamkuta ameshaolewa. Dk. Semakafu amesema mtoto wa kiume anaweza akatoka kwenye kuongoza watalii na akaja akawa na maisha bora zaidi. Amesema mtoto wa kike akidondoka kidato cha nne ndio unakuwa mwisho wa maisha yake.
Naibu katibu wa wizara ya elimu Dkt. Avemaria Semakafu (katikati) akisikiliza mpango mkakati wa shirika la (WEI) uliokuwa ukielezwa na Bi, Grace Muro (kulia)
Naibu katibu mkuu Wizara ya elimu amesema wizara imeanzisha elimu mbadala altenative education. Amesema kuna watoto tutawapeleka chuo cha maendeleo ya jamii pale Mto wa mbu kwa ajili kupata elimu mbadala. Amesema wizara imepanga kuanza na vyuo vya maendeleo ya jamii baada kuvipokea vyuo hivyo kutoka iliyokuwa wizara ya maendeleo na jamii na watoto. Amesema jambo la kwanza walilofanya katika vyuo hivyo ni ukarabati wa kutosha na kutengeneza mabweni na madarasa ya day-care. Amesema wameanzisha progaramu hiyo ya ili mtoto wa kike aweze kutimiza ndoto zake bila kumfanyia dhuluma kwa mtoto aliyemzaa.
Amesema kutakuwa na elimu ya sekondari katika vyuo hivyo lakini siyo kwa muda wa kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa nane mchana au kwa miaka minne bali mtoto atasoma kulingana na matakwa ya muda wake. Amesema hawa wasichana hatuwalazimishi wajikite katika elimu ya darasani lakini msichana anahiari kusoma katika vyuo hivyo na kupata elimu ya sekondari au ufundi au elimu zote kwa pamoja.
Dkt. Avemaria Semakafu pamoja na mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa (WEI) na watendajiwa Halmashauri ya Karatu
Dk. Semakafu amesema kwa kushrikiana na veta wameweza kutafsiri elimu ya vyuo hivyo kwa mitaala ya ngazi ya kwanza mpaka ngazi ya tatu kwa kiswahili kwa sababu baadhi ya wanafunzi wameishiria darasa la saba. Amesema wizara inashirikiana na Taasisi ya elimu ya watu wazima ili nao waanze kutoa elimu mbadala kwa watoto wetu waliokosa fursa. Mkakati wa wizara ya elimu kwa sasa hatutaki watoto wadondoke bali shule iwe mahali salama kwa vijana wa kike na wakiume. Amesema wizara sasa inajikita katika ujenzi wa mabweni ili kupunguza watoto wanaotembea umbali mrefu kwenda shule. Amesema hayo si mazingira rafiki kwa mtoto wa kike.
Wizara ikijenga mabweni inajenga mabweni ya wavulana na inajenga mabweni ya wasichana ili kuondoa vikwazo vinavyomnyima mwanafunzi kunufaika na elimu. Ameshukuru shirika la (WEI) kwa kuwatayarisha wanafunzi. Amesema ualimu ni harakati lengo letu ni kuokoa maisha, lengo letu ni kutengeneza taifa la kesho. Watoto wa kike waliochukuliwa Karatu kwenda kupata elimu mbadala Mto wa mbu wakisadiana na shirika la (wei) wataenda kuwapachachu wenzao katika chuo cha maendeleo ya jamii. Amesema shirika la (wei) linaunga mkono wizara ya elimu na linaunga mkono serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Awali Mhe.Theresia Mahongo amesema shirika la (wei) waache wasome, na Bantwana wamesaidia kuwafunza watoto kupata uelewa wa karibu juu ya haki zao. Amesema shirika la (wei) limefanya mabadiliko makubwa sana katika shule 17 ilizokuwa inafanya kazi. Program iliyolenga walimu juu ya mahusiano kati ya walimu na wanafunzi na walimu kujua kama wao ni walezi wa wanafunzi imepunguza tofauti ya awali katika shule hizo ambazo walimu walikuwa mbali sana na wanafunzi.
Ndugu Weuces Msuya wa shirika la (WEI) Mtaalamu maalum wa waache wasome amesema kuna swala la wanaume kutoelewa kwamba matendo ya ngono yanachangia kuleta mimba zisizo tarajiwa na kuleta watoto wasio na muelekeo. Wanaume wanashindwa kufahamu kwamba vitendo vya ngono ni vitendo vya majukumu. Ndugu Msuya amesema mila na desturi zetu zinalinda wanaume anapompa ujauzito mtoto wa kike na bado hakuna sheria zinazomlinda mtoto wa kike asilee mtoto mwenyewe. Wasichana 20 wameletwa katika chuo cha maendeleo ya jamii ili waweze kujiendeleza kwa elimu na lengo la (WEI) ni kuwapatia vijana wa kike elimu mbadala kwa walioshindwa kupata elimu.
Moja ya mtoto wa kike ambaye anatarajiwa kunufaika na elimu mbadala Bi, Prisca Vicent ambaye ametokea Ganako, amesema alifikia maamuzi ya kuacha shule kwa sababu alikuwa ni mgonjwa wakati huo, lakini kulikuwa na umbali mrefu kutoka nyumbani mpaka eneo la shule ilipojengwa. Anasema ilikuwa inamchukua masaa mawili mpaka masaa matatu kufika eneo la shule.
Bi prisca anasema wazazi walimpeleka kukaa kwa watu waliokaribu na eneo la shule, huko nako akakumbana na madhila kutumikishwa kazi kama mfanyakazi wa ndani. Anasema nyumba waliyompokea na kukubali kuishi nae, baba mwenye nyumba alikuwa anamtaka kimapenzi, anasema aliogopa sana kwa sababu mama mwenye nyumba angesikia angemuuwa hivyo akafanya uamuzi wa kuacha shule. Anasema alijiunga na mradi wa waache wasome mwaka jana nafasi aliyopata ya kwenda shule tena ataitumia vizuri kutimiza ndoto zake.
Naibu katibu Mkuu wizara ya elimu Sayansi na Technolojia Dkt. Avemaria Semakafu akiwakabidhi wanafunzi wa kike kwa mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii Mto wa mbu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa