• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

MAENDELEO YATALETWA NA SISI WENYEWE

Posted on: October 20th, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Wananchi lazima tuwe na ari ya kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yetu. Tukijiwekea mikakati ya kujenga zahanati lazima vitendo vyetu vitafsiri malengo ya kuwa na zahanati, hata wadau wa maendeleo wanapokuja kutusaidia basi wakute tumeshaanza ujenzi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda katika kikao cha ndani na wazee wa kimila (Malagwanani) huko Lositete. Amesema serikali imetoa kiasi cha Million 150 wilaya ya Karatu kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma  katika  zahanati ya Jobaj, Mang’ola juu, na zahanati ya Huduma. Zahanati zote hizo zimejengwa na vijiji husika amesema mpaka sasa kuna zahanati tano wilayani Karatu  ambazo ni Bashay, G-arusha, Sumawe Mahhahha na Marera tayari zimeshakamilika na zinasubiria kufunguliwa baada ya kumaliza usajili.  Ameongeza kusema Wilaya ya Karatu inapata bajeti million 450  kutoka serikalini kwa ajili ya madawa kila mwaka.

Mh. Abbas Kayanda akiwa katika kikao cha ndani na wazee wa kimila.


Akizungumzia kuhusu usambazaji  wa umeme vijijini Mh. Kayanda amesema serikali imevunja mkataba na mkandarasi wa awali wa usambazaji wa umeme (REA three) round one ambaye alitakiwa kumaliza kazi tarehe 30 mwezi wa nane baada ya kushindwa kuendana na makubaliano ya mkataba.  Hivi sasa Tanesco inafanya tathimini ya mradi mzima ili waweze kumalizia, maeneo yaliyobakia, amewahakikishia wazee wa kimila wa Lositete kwamba umeme utafika Lositete kwa sababu kijiji cha Lositete kipo ndani ya Mpango wa kusambaza umeme.  Amesema vijiji ambavyo havikuingia kwenye awamu hii vitawekwa kwenye umeme wa (Rea three round two) na utasambazwa kwenye taasisi zote za serikali kama shule zahanati na ofisi za kijiji.

Kuhusu barabara Mh. Kayanda amesema barabara ya Lositete lazima itakarabatiwa kwa sababu tayari iko kwenye bajeti ya mwaka huu. Utengenezaji  wa barabara za vijijini unasimamiwa na wakala wa barabara vijijini (Tarura) Mh. Kayanda amewashukuru wazee wa kimila kwa kudumisha hali ya  ulinzi na usalama. Amesema wazee wamekuwa imara kuwaelekeza vijana mambo ambayo serikali inawahitaji kufanya.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi wa Lositete

Pamoja na kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Kayanda alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Lositete ambao walikuwa katika mkutano wao mkuu wa kijiji. Pamoja na mambo mengine amewahidi kuendelea kushirikiana nao amesema uongozi si kuongoza peke yako lazima kushirikiana na wananchi katika kuongoza.

Awali katika salamu zao wazee wa kimila walimueleza  Mkuu wa wilaya furaha yao kwa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu ndg. Waziri Mourice aliyewaahidi wanakijiji wa Lositete kiasi cha million 7.7 kwa ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi Lositete, ukarabati wa majengo  matatu ya nyumba za walimu na kukubali kuwalipia  mshahara walimu wa ziada wapatao wanne wa muda wa miezi miwili mwezi November na Desember.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa