Wawezeshaji wa Tassaf ngazi ya taifa wameingia katika mafunzo ka njia ya vitendo, juu ya namna bora ya uendeshaji wa vikundi. Mafunzo hayo ya vitendo yatafanyika kwa mda siku mbili ili kuwajengea uwezo wa wawezeshaji wa ngazi ya wilaya ili kuongeza uelewa na kuwajengea uwezo kiutendaji.
Ndugu Masejo Songo afisa ufuatiliaji Tassaf amesema mafunzo hayo yalilenga uwezeshaji ngazi ya wilaya ili baadae wasaidie vikundi vya uwekaji na uwekezaji ngazi ya kijiji. Amesema ni matumaini kwamba mafunzo hayo hayataishia hapo yatakuwa endelevu na yatawaletea maendeleo makubwa kwa wanavikundi walio katika ngazi kijiji kwa kutoa elimu nzuri. Ndugu Masejo amesema malengo yao ni kuona wawezeshaji wanasimamia vizuri vikundi vyote vya kuweka na kuwekeza katika ngazi ya kijiji. Amesema lengo ni kusaidia wanavikundi kupata uelewa mkubwa wa kupata mikopo namna ya kuweka akiba kukopa mikopo na kuwekeza ili kuboresha maisha ya wanavikundi. Amesema mafunzo yameenda vizuri ngazi ya kijiji kwa sababu walenga wameonesha utofauti ya ufahamu walio kuwa nao kabla ya mafunzo na baada ya kupata mafunzo.
Bi, Judith Jakobo muwezeshaji ngazi ya taifa ameshukuru wawezeshaji wa wilaya kwa kupokea mafunzo vizuri. Amesema wakufunzi wa ngazi ya wilaya wameweza kutoa elimu vizuri katika ngazi ya kijiji. Kazi hiyo ya mafunzo kwa muda wa siku tano imekuwa na ufanisi mkubwa, amesema kabla ya mafunzo walengwa wengi walikuwa hawatumii fedha kwa malengo yaliyokusudiwa. Mafunzo haya yamelenga kujenga uelewa mkubwa kwa walenga kama kujifunza kutunza na kujaza vitabu vya kumbukumbu ya fedha. Kujifunza kutunza fedha zao na kujua fedha zao jinsi gani zitakavyotoka na jinsi gani zitavyorudi na jinsi gani watafanya mgawanyo wao wa fedha kwa namna walivyoweka. Bi, Judith amesema wamewafundisha pia namna ya kuaanda mpango kazi katika vikundi vyao.
Bi, Judith amesema vikundi vya kuweka na kuwekeza vimesaidia sana walengwa kujikwamua kiuchumi. Amesema kuna walengwa wamepata mitaji ya kuwekeza katika kilimo, mifugo na kupata uwezo wa kuwasaidia kununua vifaa vya shule kwa watoto wao.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa