Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Mzee mkongea Alli, amesema mwenge wa uhuru uliasisiwa na Baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwaka huu ni mwaka wa ishirini tangu Baba wa taifa alipofariki. Amesema kwa kuenzi mchango wake ndio maana wamedhamiria kufanya kazi bila kuchoka.
Ndugu Mkongea amesema pia wataendelea kupigana na adui ujinga maradhi na umaskini.Ndugu Mkongea amesema kauli mbiu ya mwenge mwaka huu ni “maji ni haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa” Ndugu Mzee Mkongea amesema maji ni rasilimali muhimu sana. Kupitia ilani ya chama cha mapinduzi (2015-2020) kufikia mwaka 2020 itahakikisha wananchi wanaoishi vijijini wanapata maji kwa asilimia themanini na tano. Ndugu Mkongea amesema miradi ipatayo 1659 imeweza kukamilishwa kwa upande wa vijijini. Ndugu Mkongea amesema wananchi wanoishi mjini ifikapao 2020 watapata maji kufikia aslimia tisini na tano. Miradi ipatayo 124 imekamilishwa kwa wakati kwa kipindi cha (2016-2018) sera za kimkakati za kuchimba visima virefu na vikubwa ambavyo vimegharimu shilingi billion kumi na nane za Kitanzania.
Ndugu Mkongea amesema mwezi wa kumi serikali inaingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kusikiliza sera za wagombea na kupiga kura. Amewaomba wananchi kujitokeza kugombea na pia amesihi wananchi kuchagua viongozi bora wenye hofu ya mungu. Viongozi wa serikali za mitaa wanachangia katika shughuli za maendeleo kutunza mazingira. Serikali za mitaa zinachangia sana katika kutunza ulinzi na usalama. Ndugu Mkongea amesema kwenye uchaguzi kuna kushinda na kushindwa ni vyema atakayeshindwa kukubali matokeo na kutoa ushirikiano kwa aliyeshinda.
Ndugu Mkongea amesema bado swala la maambukizi ya ukimwi ni changamoto, wastani wa maambukizi ni asilimia nne nukta saba. Mkoa unaongoza kwa maambukizi ni mkoa wa Njombe 11.4% na mkoa wa Iringa unafuata 11.3 % mkoa wa Mbeya unafuata 9.3% na mkoa wa Mwanza unafuata 7.2 %. Ndugu Mkongea amesema maambuki mapya kwa mwaka ni watu 81000 na kwa sasa kuna watu wanasadikiwa1400,000 wanaishi na virusi vya ukimwi. Ndugu Mkongea amesema mambukizi ya ukimwi ni changamoto kwa nchi. Ameombwa wananchi kujitokeza kupima amesema ukibainika utapewa ushauri nasaha. Ameombwa wananchi wasiwanyanyapae watu walioadhirika na ukimwi amesema kuishi na virusi vya ukimwi siyo mwisho wa maisha.
Ndugu Mkongea amesema mwenge bado unaendelae na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya. Ameomba wananchi kushirikiana pamoja, dhidi ya vita hiyo ya madawa ya kulevya chini ya kauli mbiu, Tujenge maisha yetu, jami yetu, Utu wetu, bila matumizi ya dawa za kulevya. Ndugu Mkongea amesema bado mbio za mwenge zinaendeleza mapambano dhidi ya rushwa chini ya kauli mbiu kataa rushwa jenga Tanzania. Mwenge wa uhuru unaendelea na mapambano dhidi ya malaria chini ya kauli mbiu mimi niko tayari kutokomeza malaria, wewe je ?
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa