Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ametembelea eneo linalojengwa Hospitali ya wilaya ya karatu kijiji cha Changarawe. Ziara hiyo ililenga kukagua na kujionea hatua za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Karatu.
Mhe. Mrisho Gambo amepongeza mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kusaidia kuanzisha ujenzi wa Hospital ya wilaya. Amesema serikali ina mpango wa kujenga hospitali za wilaya nchi nzima katika mpango huo wilaya ya Karatu ilikuwa imewekwa kwenye hatua za baadae. Lakini mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro ambayo ni taasisi ya serikali ilisaidia kuanzisha ujenzi wa hospitali ya wilaya kwa majengo matatu jengo la wagonjwa wa nje, jengo la maabara na jengo la utawala. Mamlaka walitoa kiasi cha million 500 kwa kuanzia mwaka wa fedha uliopita na wameahidi kutoa million 100 katika mwaka huu wa fedha kusaidia ujenzi wa hospitali ya wilaya. Mhe. Gambo amesema bado mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na timu yake wameahidi kuendelea kuchangia zaidi kwenye ujenzi huo wa hospitali ya wilaya ya Karatu.
Mhe. Mrisho Gambo akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Karatu katika kijiji cha changarawe.
Mhe. Gambo amesema ujenzi wa hospitali ya wilaya utasaidia wakazi wa wilaya zote mbili za ngorongoro na Karatu. Mhe. Gambo amesema mkoa wa arusha ulikuwa na hospitali mbili tuu za wilaya. Hospitali zilizokuwepo zilikuwa ni hospitali ya wilaya ya Monduli na Hospitali ya wilaya ya Arumeru. Amesema hivi sasa wilaya nne za mkoa wa Arusha zinajenga hospitali ya wilaya, amesema haya ni mafanikio makubwa yaliyofanywa na Mhe. Rais, Dkt, John Pombe Magufuli. Amesema serikali imewekeza katika huduma za watu, serikali imejenga na kukarabati kituo cha afya double D, kituo cha afya kambi ya simba, kituo cha afya Endabash. Amesema gharama za matibabu ya afya zilikuwa kubwa mno, katika vituo vya afya vya watu binafsi, mathalani mama mjamzito akitaka kujifungua kwenye hospital binafsi gharama si chini ya laki nne. Vituo vya afya vya serikali kujifungua ni bure, hiyo ni ishara kwamba mambo yanatekelezeka kivitendo.Mhe. Gambo amesema miundo mbinu yote ya msingi kama maji umeme na barabara ya lami mpaka kwenye hospitali ya wilaya itawekwa.
Mhe. Mrisho Gambo katikati akipokea maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya dkt Mustafa Waziri upande wa kulia
Mwenyekiti wa bodi ya Hifadhi ya Ngorongo Prof, Abiud Kaswamila amesema amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya. Amefurahi kusikia pia kwamba mwaka huu wa fedha TAMISEMI imetoa kiasi cha shilingi million 500 katika ujenzi wa hospitali ya wilaya. Mwenyekiti ameomba Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo kuendelea kuhamasisha ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Karatu kwa kuhusisha makampuni binafsi na wadau wanaojihusisha na mambo ya utalii kuchangia ujenzi wa hospital ya wilaya.
Injinia wa Halmashauri ndugu Venance Malamla amesema Halmashauri imetenga kiasi cha sh.40 kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospital ya wilaya. Ujenzi wa hospital ulianza tarehe 8 /4 mwaka 2019 na ulitarajiwa kumalizika 8/8 2019. Mhandisi amesema jengo la wagonjwa wa nje linajengwa kwa gharama ya million 50 laki nane na hamsini ambalo liko chini ya Damiano John ambaye ameingia mkataba wa kujenga jengo hilo. Kiasi cha million 45 laki saba na thelathini kitatumika kujenga jengo la maabara kwa mkataba na Damiano John. Jengo la utawala litajengwa na Alex Obadia Tenga ambaye ameingia mkataba wa kujenga kwa gharama ya million 51 miatatu themanini. Mhandisi amesema jumla ya ujenzi kwa majengo yote matatu ni kiasi cha shilling million 147 mia tisa sitini hadi ujenzi utakapo kamilika. Mhandisi Venance amesema mpaka sasa ujenzi wa majengo yote matatu umefikia kiwango cha 37%
Mafundi wakiwa wanaendelea na ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa